Kiungo mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa la Uingereza Jadon Sancho huenda napitia wakati mgumu sana katika maisha yake. Hii ni baada ya kuondoa picha ya utambuisho wake kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuibadilisha na picha nyeusi.
Kando na hili, Sancho pia alifuta picha zote kwenye ukurasa huo wake wa Instagram ulioko na wafuasi zaidi ya milioni 9, na hili limezua gumzo na wasiwasi baina ya mashabiki wake.
Mchezaji huyo ambaye tangu kuigura Borussia Dortmund miaka miwili iliyopita na kujiunga na timu ya Manchester United, viwango vyake vya mchezo vimekuwa vikidorora kwa kasi ya 5G, jambo ambalo lilimfanya kukosa nafasi katika timu ya taifa la England kuelekea michuano ya kombe la dunia.
Mpaka kufikia sasa ligi zote barani Ulaya zilipochukua likizo fupi ili kupisha michuano ya kombe la dunia, Sancho ana mamabo matatu tu na asisiti moja katika mashindano yote.
Baada ya kutemwa nje ya kikosi cha wachezaji 26 waliosafiri kuenda Qatar kushiriki kombe la dunia, mashabiki wa soka kwenye mitandao ya kijamii walimgeuza Sancho kuwa kichekesho huku wengine wakimtania jinsi alivyoshuka ngazi kutoka mchezaji wa kutegemewa hadi yule wa kusahaulika kabisa na meneja Gareth Southgate wa timu ya taifa ya England.
Baada ya mabadiliko hayo makubwa kwenye ukurasa wake wa Instagram, mashabiki wenye wasiwasi walijitokeza kuonesha mashaka yao na kitendo hicho huku wengine wakisema huenda anapitia msongo wa mawazo si tu kutokana na kutoitwa kwenye timu ya taifa bali pia kutokana na mfadhaiko wa kupoteza ubora wake uwanjani.
“Natumai Sancho ako sawa ak!” mmoja kwa jina LJ Xmes aliandika Twitter.
“Sancho amekuwa akipambana na kunyanyapaliwa kutokana ubaguzi wa rangi, na pia kufiwa kwa mmoja wa wanafamilia wake. Hapa kati amekuwa aking’ang’ana kupata uzoefu katika ligi hii mpya kando na kuchezeshwa kwa mifumo tofauti na makocha 4 chini ya mwaka mmoja. Huu ni mng’ang’ano mbaya sana wa kisaikolojia kutoka kwa kijana huyu wa miaka 22 pekee,” mwingine kwa jina Vhidalokaa alimtetea.
“Kwa kweli Sanchi angefaidi mno kama angechagua klabu yenye inacheza mchezo wa soka ambao alikuwa amezoea au kutafuta klabu yenye ingemlipa mshahara wa kima cha chini ili awe na matrumaini machache ya kile anakifanyia kazi na pia kuwa na uchu wa kujituma kutaka zaidi,” mwingine alisema.