Saudi Arabia hii leo imewashangaza wengi kwa ushupavu na ujasiri wao baada ya kuwalaza washindi mara mbili wa kombe la Dunia Argentina katika mechi ya kwanza ya Kundi C mjini Lusail.
Saudia ambayo imeorodheshwa ya 51 duniani, ingeweza kucharazwa katika kipindi cha kwanza huku Lionel Messi akifunga bao la kwanza huku magoli mengine matatu yaliofungwa na Argentina yakikataliwa kwa kuotea.
Lakini Saudi Arabia iligeuza mchezo katika kipindi cha pili ndani ya dakika 10 baada ya muda wa mapumziko ambapo , Saleh Al-Shehri alisawazisha naye Salem Al Dawsari kuwaweka.
Magoli hayo yaliifanya Argentina kuongeza juhudi wakitafuta magoli ya kusawazisha lakini ,mabeki wa saudia hawakuwaruhusu Messi na wenzake kutamba mbele ya goli wao.
Matokeo hayo yameimarisha matumaini ya Saudia huku Argentina wakiwachwa na kibarua cha kujizatiti katika mechi zijazo ili kumpa Messi mwisho ufaao wa Kombe la Dunia.