Rais wa shirikisho la soka nchini Cameroon Samuel Eto'o amejitokeza na kuomba radhi kwa kuhusiana na ugomvi na mwanamume mmoja nje ya uwanja wa Kombe la Dunia nchini Qatar.
Katika taarifa yake, Eto'o alikashifu uchokozi usiokoma na unyanyasaji wa kila siku wa baadhi ya wafuasi wa Algeria.
"Baada ya mechi ya Brazil na Korea Kusini, nilikuwa na ugomvi mkali na mtu ambaye pengine alikuwa mfuasi wa Algeria," Eto'o alisema.
"Ningependa kuomba radhi kwa kushindwa kujizuia na kujibu kwa njia ambayo hailingani na utu wangu. Naomba radhi kwa umma kwa tukio hili la kusikitisha."