logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pep Guardiola: Halaand 'anastahili heshima aliyopewa'

Amevunja rekodi ambayo awali alimuweka katika kiwango sawa na Alan Shearer na Andy Cole.

image
na Samuel Maina

Michezo04 May 2023 - 05:43

Muhtasari


  • •Kufunga bao la 3 - 0 dhidi ya West Ham kwa Haaland kunamaanisha kuwa sasa ana mabao 35 ya ligi katika msimu.

Pep Guardiola amedai lifanyike gwaride la heshima kwa ajili ya wachezaji wake na wafanyakazi wa klabu hiyo kuadhimisha bao la rekodi Erling Haaland la Primia Ligi – kumuonyesha mshambuliaji huyo jinsi mafanikio aliyoyapata yalivyo maalumu.

Kufunga bao la 3 - 0 dhidi ya West Ham kwa Haaland kunamaanisha kuwa sasa ana mabao 35 ya ligi katika msimu.

Amevunja rekodi ambayo awali alimuweka katika kiwango sawa na Alan Shearer na Andy Cole.

"Wakati kuna tukio maalumu, tunapaswa kuonyesha ni kwa jinsi gani lilivyo maalumu," amesema Guardiola.

Wachezaji wenzake wa Manchester city, pamoja na Guardiola na wahudumu wengine wa klabu hiyo waliokuwa katika chumba cha mavazi, walijipanga mstari kumpatia heshima Haaland alipokuwa njiani kuelekea katika chumba cha kubadilisha mavazi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved