Timu ya taifa ya Harambee Stars imeondoka nchini siku ya Jumatatu ili kushiriki michuano ya mataifa manne inayoendelea nchini Mauritius.
Kikosi cha wachezaji 23 na benchi la ufundi waliondoka nchini kwa ndege shirika la ndege la Kenya Airways saa 10 jioni.
Timu hiyo inatarajiwa kuwasili Mauritius saa tisa jioni baada ya kukosa kusafiri siku ya Jumamosi kwa sababu yakukosekana kwa ndege iliyokuwa ikielekea nchi ya Mauiritius.
Stars ilipaswa kuwa imewasili Mauritius kufikia Ijumaa wiki jana na ilipaswa kucheza mechi ya kwanza dhidi ya Djibouti Jumamosi.
Wakiwa wamekosa mechi ya ufunguzi, Kenya sasa itamenyana na Pakistan na mwenyeji Jumatano na Jumapili mtawalia.
Kabla ya kuondoka kwa timu hiyo, kocha Engin Firat alidokeza kuwapa wachezaji wapya nafasi ya kuchezea timu hiyo ya taifa kwa mara ya kwanza ili wawe na hisia za soka la kimataifa.
“Tunataka kuwapa wachezaji wapya nafasi ya kuwa na muda zaidi na kujaribu mambo mapya. Wachezaji watano ambao walikuwa kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Iran hawapo kwenye timu na hakika hii itakuwa na hiyo itakuwa na athari kwetu," Firat alisema.
Baadhi ya wachezaji wapya katika kikosi hicho ni pamoja na Luke Otiala, Moses Shumah, Byrne Omondi, Joseph Mwangi, Benson Omala, na Charles Ouma.
Kikosi hicho kiliwajumuisha walinzi Ian Otieno( Zesko, Zambia), Bryne Odhiambo (KCB) ,Brian Bwire (Tusker), Simon Masaka (Sofapaka).
Mabeki: Joseph Okumu (Gent, Belgium), Daniel Anyembe (Viborg, Denmark), Eric Ouma (AIK, Sweden) Collins Shichenje (KUPS), Daniel Sakari (Tusker), David Ochieng (Kenya Police), Abud Omar (Kenya Police), Mohamed Siraj (Bandari), Kevin Luke Otiala (Kariobangi Sharks), Robinson Kamura (Kakamega Homeboyz).
Viungo: Amos Nondi (Ararat, Armenia), Richard Odada (Philadelphia Union, USA), Kenneth Muguna (Azam, Tanzania), Teddy Akumu (Sagan Tosu, Japan), Alvin Mangeni (Kenya Police), Clifton Miheso (Kenya Police), Charles Ouma (Kenya Police), Abdallah Hassan (Bandari), Joseph Mwangi (Nzoia Sugar), Alpha Onyango (Gor Mahia), Bonface Omondi- (Gor Mahia), Victor Omune (AFC Leopards ).
Washambulizi: Michael Olunga (Al Duhail, Qatar), Masoud Juma (Difaa El Jadidi, Morocco), Moses Shummah (Kakamega Homeboyz), Benson Omalla (Gor Mahia).
Mauritius, Kenya, Djibouti na Pakistan zinashiriki michuano hiyo iliyoanza kuanzia Juni 11 hadi Juni 18.