logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ligi ya Saudia yazidi kuwa yenye mvuto, Steven Gerrald akitwikwa jukumu la ukufunzi

Sehemu kubwa ya uchezaji wa Gerrard aliitumia Liverpool, ambayo alicheza zaidi ya mechi 700.

image
na Davis Ojiambo

Michezo14 June 2023 - 06:37

Muhtasari


  • • Akiwa Villa Gerrard alishinda 13, sare nane na kupoteza mechi 19 kati ya 40 alizoongoza katika timu hiyo.
  • • Kabla ya hapo alishinda taji la Ligi Kuu ya Uskoti akiwa na Rangers katika kampeni ya 2020-21.
Steven Gerrald apata kazi ya ukufunzi Saudi Arabia.

Gwiji wa Liverpool Steven Gerrard anaripotiwa kuteuliwa kuwa meneja mpya wa Al-Ettifaq.

Gerrard amekuwa hana kazi tangu alipotimuliwa Aston Villa Oktoba mwaka jana.

Kulingana na mwanahabari Romain Molina, Gerrard amewasili Saudi Arabia huku akijiandaa kuchukua kazi ya Al-Ettifaq.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 43 alihusishwa na wadhifa huo wikendi na sasa inaonekana anakaribia kuteuliwa.

Al-Ettifaq walimaliza katika nafasi ya saba msimu huu kati ya timu 16.

Gerrard anaweza kuwa jina la hivi punde zaidi kuhamia Saudi Arabia, huku Cristiano Ronaldo akijiunga na Al-Nassr mwezi Januari.

Karim Benzema aliondoka Real Madrid na kwenda Al-Ittihad na huenda akajiunga na kiungo wa Chelsea, N'Golo Kante.

Al-Hilal ilijaribu kumsajili Lionel Messi lakini nyota huyo wa Paris Saint-Germain alichagua kuhamia Inter Miami ya Marekani badala yake.

Akiwa Villa Gerrard alishinda 13, sare nane na kupoteza mechi 19 kati ya 40 alizoongoza katika timu hiyo.

Kabla ya hapo alishinda taji la Ligi Kuu ya Uskoti akiwa na Rangers katika kampeni ya 2020-21.

Gerrard hivi majuzi alihusishwa na kibarua cha Leicester, huku Foxes wakitafuta meneja mpya kuchukua nafasi ya Dean Smith kufuatia kushushwa daraja.

Sehemu kubwa ya uchezaji wa Gerrard aliitumia Liverpool, ambayo alicheza zaidi ya mechi 700.

Alirejea Liverpool kuanza maisha yake ya ukocha akiwa na timu za vijana za klabu hiyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved