Vigogo wa Ligi ya Premier Manchester City wametangaza kumsajili kiungo wa Chelsea Mateo Kovacic.
Huku meneja Pep Guardiola akiendelea kuimarisha safu yake ya kati, kutua kwa Kovacic ugani Etihadi ni bayana kuwa kuna baadhi ya wachezaji walio katika hatari ya kuiaga klabu hiyo.
Naodha Ilkay Gundogan, ambaye ambaye alisajiliwa kutoka Borussia Dortmund, Guardiola alipotua Man City, amekuwa kiungo wa maana sana ambapo amesaidia klabu hiyo kunyakua mataji kadha, yakiwemo “ Treble” katika msimu uliotamatika mwezi Juni. Kwa ujumla tangu 2016 hadi 2023, amechezea City jumla ya mechi 304 na kufunga mabao 60.
Klabu ya Man City imejaribu juu chini kumshawishi Mjerumani huyo kuongeza kandarasi ila bado wapo katika mtafaruku ambapo siku za hivi karibuni amehusishwa na miamba wa La Liga, Barcelona.
Pep Guardiola, awali alisikitishwa na kauli ya Gundogan kutaka kuondoka kwenda Barcelona, ambapo alikiri kuwa iwapo nyota huyo ataondoka, basi watakuwa wamempoteza mchezaji wa maana sana, akidai kuwa Barcelona watakuwa wenye bahati kumpata mchezaji huyo.
“I wish he stays. If he Leaves we are going to lose a fantastic player. If Barcelona will manage to sign him, they will have a great player, what a player! (Natumai atadumu. Iwapo ataenda tutampoteza mchezaji mahiri sana. Barcelona watakuwa wamemsajili mchezaji mahiri.)”Pep alieleza BT Sports.
Katika msimu huu wa joto, City wanalenga kuwasajili Kovacic na Josko Gvardiol huku pia wakiwa na wasiwasi wa kudumu kwa wachezaji sita wakiwemo Gundogan, Bernado Silva, Laporte, Kyle Walker,Mahrez na Cancelo.
Kuondoka kwa naodha huyo katika ligi ya Premier, ni ishara kuwa City itabidi kumchagua nahodha mwingine atakayeingoza msimu ujao wa 2023/2024.