logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hongera! Beatrice Chebet ashinda medali ya dhahabu katika mbio za Diamond league

Katika hali ngumu ya hewa alirekodi wakati wake bora wa msimu wa dakika 14 sekunde 36.52.

image
na Samuel Maina

Michezo04 July 2023 - 03:54

Muhtasari


  • •Beatrice Chebet aliongoza watatu bora Afrika katika mbio za mita 3000 kwa wanawake huko Diamond League mjini Stockholm, Uswidi Jumapili.

Mkenya Beatrice Chebet aliongoza watatu bora Afrika katika mbio za mita 3000 kwa wanawake huko Diamond League mjini Stockholm, Uswidi Jumapili.

Katika hali ngumu ya hewa alirekodi wakati wake bora wa msimu wa dakika 14 sekunde 36.52.

Waethiopia Lemlem Hailu na Medina Eisa waliibuka wa pili na wa tatu Ethiopia na kumiliki medali katika mbio za mita 1500 kwa wanawake, huku Freweyni Hailu akiongoza kwa muda wa 4:02.31.

"Ushindi ni mkubwa lakini ushindani haukuwa mzuri kutokana na hali ya hewa. Lakini tunapaswa kukabiliana na hali zote," Hailu amenukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema.

Mafanikio mengine ya Afrika ni pamoja na:

  • Akani Simbine wa Afrika Kusini ameshinda mbio za mita 100 kwa wanaume
  • Zakithi Nene wa Afrika Kusini ameshinda mita 400 kwa wanaume
  • Djamel Sedjati wa Algeria ameshinda mbio za mita 800 kwa wanaume
  • Huku Tobi Amusan wa Nigeria akishinda mbio za mita 100 kwa wanawake

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved