logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Binti wa Eto'o ataka mchezaji huyo wa zamani kufungwa jela kwa kukataa kumpa matunzo

Erika, 22, alizaliwa na mpenzi wa zamani wa Eto'o Adileusa de Rosario

image
na Davis Ojiambo

Michezo06 July 2023 - 04:05

Muhtasari


  • • Hata hivyo, hatimaye Eto'o alimtambua bintiye mnamo Februari 2022.
  • • Alitakiwa kumlipa malipo ya ziada ya kila mwezi, kwa kuwa hali yake ya kifedha si nzuri.
Bintiye ataka mchezaji wa zamani wa Camroon kufungwa.

Binti wa nguli wa Barcelona Samuel Eto’o anataka afungwe jela kwa kushindwa kulipa karo ya mtoto ya Euro 90,000., kiasi sawa na shilingi za Kenya Milioni 13.74, jarida la Sportskeeda limefichua.

Kulingana na gazeti la Uhispania la Sport, nguli wa Barcelona Samuel Eto'o anaweza kufungwa jela baada ya kushindwa kumlipa bintiye Erika de Rosario malipo ya kila mwezi ya Euro 1,400 kwa miaka mitano.

Erika, 22, alizaliwa na mpenzi wa zamani wa Eto'o Adileusa de Rosario. Gwiji huyo wa soka wa Cameroon, rais wa sasa wa shirikisho la soka nchini mwake, alichumbiana na Adileusa wakati akiwa mchezaji wa Real Madrid katika miaka ya 90.

Hata hivyo, hatimaye Eto'o alimtambua bintiye mnamo Februari 2022. Alitakiwa kumlipa malipo ya ziada ya kila mwezi, kwa kuwa hali yake ya kifedha si nzuri.

Wakati Eto'o anaishi maisha ya utele, hakumlipa binti yake pesa ya kumlea kwa miaka mitano, kumaanisha kwamba anadaiwa karibu €90,000. Wakili wa Erika, Fernando Osuna, alisema (kama ilivyo kwa El Diario de Sevilla):

"Anadaiwa zaidi ya miaka mitano ya pensheni kwa binti yake na anaendelea kukaidi haki. Uchumi wa Erika ni dhaifu, wakati Eto'o anaishi maisha ya anasa."

Osuna aliongeza:

"Anaweza kuhukumiwa kwa hali mbaya ya matumizi mabaya ya madaraka, kutokana na ubora wake kiuchumi kuliko Erika."

Kesi kuhusu kesi hiyo itafanyika mjini Madrid, Osuna alisema, huku mshambuliaji wa zamani wa Barcelona Samuel Eto'o akijikuta kwenye maji ya moto.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved