logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Serikali Somalia yaomba radhi kwa kupeleka mkimbiaji 'anayekimbia taratibu' kwenye mbio za kimataifa

"Kilichotokea leo haikuwa uwakilishi wa watu wa Somalia... tunaomba radhi kwa watu wa Somalia," Waziri alisema.

image
na SAMUEL MAINA

Michezo03 August 2023 - 03:52

Muhtasari


  • •Waziri wa Michezo Mohamed Barre Mohamud alitaja tukio hilo kuwa la aibu. "Kilichotokea leo haikuwa uwakilishi wa watu wa Somalia... tunaomba radhi kwa watu wa Somalia," alisema.

Waziri wa michezo wa Somalia ameomba radhi baada ya mshiriki mwanamke katika mbio za kimataifa za mita 100 kuonekana akikimbia taratibu kiasi kwamba watu wanahoji aliwezaje kuchaguliwa.

Katika mashindano ya michezo ya vyuo vikuu katika mji wa Chengdu nchini China, Nasra Abubakar Ali alitumia karibu sekunde 22 kumaliza mbio hizo - karibu mara mbili ya muda aliyoutumia mshindi.

Katika video ya tukio hilo, ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii, mwanariadha huyo wa Somalia alionekana kukimbia kama sio mwanariadha, taratibu na kuonekana kama vichekesho.

Waziri wa Michezo Mohamed Barre Mohamud alitaja tukio hilo kuwa la aibu. "Kilichotokea leo haikuwa uwakilishi wa watu wa Somalia... tunaomba radhi kwa watu wa Somalia," alisema.

Inaelezwa kuwa ukweli wa kwamba hakuwa na uzoefu wa kushindana umewafanya baadhi ya Wasomali kushangaa kwa nini alichaguliwa.

Kama kilichofanyika ni kupata umaarufu na kujulikana inaelezwa kwenye mitandao kwamba, ameshinda sawa na medali ya dhahabu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved