logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kipchoge athibitisha kushiriki mbio za Berlin mwezi huu wa Septemba

mwanariadha wa mbio za maasafa marefu Eliud Kipchoge kutangaza kushiriki mbio na hana imani  ya kushinda

image
na Davis Ojiambo

Michezo11 September 2023 - 13:22

Muhtasari


  • • Nyota wa mbio kutangaza kuwa ana imani ya kushida mbio za Berlin msimu huu.
  • • Rekodi ya mwaka jana, Kipchonge alishusha rekodi yake ya dunia hadi 2:01:09.
alimaliza wa sita katika Boston Marathon.

Eliud Kipchoge ameweka wazi kwamba atakuwepo katika mbio za Berline mwezi huu na kuwa yuko tayari na amejiadaa kwa msimu huu ambapo anasema kuwa yuko tayari na amefanya mazoezi ya kutosha .

Mshindi huyo wa medali ya dhahabu mara mbili ya Olimpiki alitangaza kwamba yuko sawa kwenye mbio za Berlin marathoni semptemba 24 .

"Lazima nirudi kwenye nafasi yangu maalum," alisema kwenye mtandao wa instagram.

Kipchoge amekimbia mbio za Berlin Marathon mara tano ukiwemo  ushindi mara nne, lakini anafahamika zaidi kwa kuweka rekodi ya dunia huko mara mbili.

Rekodi ya mwaka jana, Kipchonge alishusha rekodi yake ya dunia hadi 2:01:09.

Rekodi ya dunia ya marathoni ya wanaume imevunjwa mara nane. Mashindano yote nane yamekuwa Berlin na hakuna mwanamka akiyeweka rekodi mbali tu ile ya Naoko Takashashi.

Tangazo la kipchoge linakuja baada ya utendaji wake wa kutatanisha katika mbio za Boston marathon mwezi Aprili, ambapo alififia kutoka kwa kundi la waongozaji hadi kumaliza wa sita

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 amesema anataka  kushinda mbio hizo za dunia za marathon katika chapisho la ukurasa wake wa instagram  kipchoge kwamba kukimbia Berlin ni mbali na lengo lake la muda mrefu la kujiandaa kwa Olimpiki ya Paris 2024.

 

Mbali na Kipchoge kwa upande wa wanadada na ambao watashiriki mashindano haya ni pamoja na Sheila Chepkirui ,Margaret Wangare.

Kwa upande wa wanaume ni akiwemo bigwa Eliud Kipchoge,Amos Kipruto,Mark  Korir,Josphat Boit,Philemon Kiplimo, Abel Kipchumba,Silas Sugut ,Dominic Nyairo and Ronald Korir.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved