logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hatimaye Chelsea wapata mdhamini wa jezi baada ya kuanza msimu bila

Hata hivyo, inatarajiwa wadhamini wapya watakuwa tayari kushiriki katika mchezo ujao wa The Blues.

image
na Davis Ojiambo

Michezo27 September 2023 - 07:10

Muhtasari


  • • Hata hivyo, inatarajiwa wadhamini wapya watakuwa tayari kushiriki katika mchezo ujao wa The Blues wa Ligi Kuu dhidi ya Fulham Jumatatu usiku.
Chelsea bila mfadhili

Baada ya vuta nikuvute baina ya klabu ya Chelsea na uongozi wa ligi kuu ya Premia Uingereza kuhusu makubaliano ya Infinite Athlete – kampuni ambayo ilikuwa imekubaliana na timu hiyo kufadhili jezi zao, hatimaye imeonekana makubaliano hayo yako karibu kuzaa matunda.

The Blues wamecheza mwezi wa ufunguzi wa msimu bila mfadhili mkuu kwenye jezi zao baada ya ushirikiano na Three kukamilika mwishoni mwa msimu wa 2022/23.

Mfumo wa utiririshaji wa Paramount na kampuni ya kamari ya mtandaoni ya Stake wote walikuwa na nia ya kuwa wafadhili wa Chelsea, lakini kila dili lilishindikana.

Kutokana na hali hiyo, Chelsea walibaki wakisubiri kupata makubaliano mapya ya udhamini ili wavae jezi zao, huku Infinite Athlete wakiibuka kama chaguo.

Hata hivyo, makubaliano yaliyofikiwa yalicheleweshwa kwa kuwa kampuni hiyo ilitaka kupata kibali cha Ligi Kuu na ambayo sasa inaonekana kuwa imetolewa.

Kwa mujibu wa Telegraph, Chelsea wamepewa kibali cha Ligi Kuu ya Uingereza kwa Infinite Athlete kuwa mdhamini mpya wa jezi za klabu hiyo.

Ripoti hiyo inabainisha kuwa dili hilo lina thamani ya pauni milioni 40 lakini makubaliano ya mwisho hayajafikiwa kwa wakati kwa Infinite Athlete kuwa kwenye jezi za Chelsea kwenye Kombe la Carabao dhidi ya Brighton.

Hata hivyo, inatarajiwa wadhamini wapya watakuwa tayari kushiriki katika mchezo ujao wa The Blues wa Ligi Kuu dhidi ya Fulham Jumatatu usiku.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved