Kipimo cha mchezaji wa kiungo cha kati wa Juventus Paul Pogba ambacho hakikufaulu kimethibitishwa baada ya sampuli yake ya pili kukutwa dawa za kusisimua misuli
Pogba, 30, alisimamishwa kazi kwa muda mwezi uliopita baada ya sampuli yake ya awali kupata viwango vya juu vya testosterone kwenye mfumo wake.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alichaguliwa kwa majaribio ya kubahatisha baada ya ushindi wa Juve wa mabao 3-0 dhidi ya Udinese mnamo tarehe 20 Agosti, wakati alikuwa mchezaji wa akiba ambaye hajatumiwa.
Iwapo atapatikana na hatia ya kutumia dawa za kusisimua misuli, anaweza kupigwa marufuku kati ya miaka miwili hadi minne.