logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tazama ratiba ya mechi zijazo za mashindano ya African Football League

Washindi wa robo fainali baadaye watapangwa kwa nusu fainali ya shindano hilo.

image
na Samuel Maina

Michezo22 October 2023 - 13:19

Muhtasari


  • •TP Mazembe ya Kongo watacheza dhidi ya Esperance Tunis ya Tunisia kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Benjamin Mkapa saa kumi na mbili jioni.
  • •Washindi wa robo fainali baadaye watapangwa kwa nusu fainali ya shindano hilo.

Ligi ya Soka ya Afrika (AFL) ingali inaendelea vyema huku mashindano hayo sasa yakiingia siku ya tatu mnamo Jumapili, Oktoba 22.

Huku mechi mbili zikiwa tayari zimechezwa, matokeo yamedokeza pambano linaloonekana kuvutia sana.

Mechi ya ufunguzi kati ya Simba S.C ya Tanzania na Al Ahly ya Misri iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Benjamin Mkapa siku ya Ijumaa ilimalizika kwa mabao 2-2 huku mabao mengi yakishuhudiwa katika kipindi cha pili cha mchuano huo.

Siku ya Jumamosi, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini iliichapa Petro Atletico ya Angola mabao 2-0 kwenye uwanja wao wa nyumbani, Estádio 11 de Novembro mjini Luanda, Angola.

Jumapili itashuhudia vilabu vinne uwanjani huku TP Mazembe ya Kongo wakicheza dhidi ya Esperance Tunis ya Tunisia kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Benjamin Mkapa saa kumi na mbili jioni.

Mechi ya pili ya siku itachezwa saa tatu usiku ambapo Enyimba ya Nigeria itaikaribisha Wydad Casablanca ya Morocco kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Godswill Akpabio mjini Uyo.

Al Ahly itaikaribisha Simba S.C kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo nchini Misri kwa mechi ya mkondo wa pili siku ya Jumanne saa kumi na moja jioni huku Mamelodi Sundowns ikicheza mechi ya mkondo wa pili dhidi ya Petro Atletico Uwanja wa Loftus Versfeld saa mbili usiku wa siku hiyo hiyo.

Esperance Tunis itamenyana na TP Mazembe kwa mechi ya mkondo wa pili kwenye uwanja wa Stade Olympique de Radès siku ya Jumatano saa kumi na mbili jioni. Siku hiyo hiyo, Wydad ya Morrocco itamenyana na Enyimba ya Nigeria kwa mechi ya mkondo wa pili Uwanja wa Stade Mohamed V saa tatu usiku.

Washindi wa robo fainali baadaye watapangwa kwa nusu fainali ya shindano hilo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved