Alipokuwa akizungumzia suala la kwanini Manchester City ni bora zaidi kuliko Manchester United, Pep Guardiola alikuwa makini kumheshimu na kumlinda meneja mwenzake Erik ten Hag.
Lakini katika kuzungumzia klabu yake, Guardiola bado aliweza kuelezea kwa njia isiyo ya moja kwa moja hali ya sasa ya wapinzani wake wa jiji.
"Nilisema mara nyingi tuko katika mwelekeo mmoja - mwenyekiti, Mkurugenzi Mtendaji, mkurugenzi wa michezo, meneja na wachezaji," alisema.
“Tunafanya makosa, lakini tunaposhindwa au mambo hayaendi sawa hatuko hapa kumlaumu mtu, tunaona tu nini cha kufanya ili kuwa bora na kutafuta suluhu.
"Katika msimu wangu wa kwanza, hatukushinda. Mwenyekiti hakulalamika, aliniunga mkono bila masharti. Tulipopoteza fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Chelsea niliumia sana. Mwenyekiti wangu alisema, 'Njoo, tuangalie , tufanye nini ili kupata ushindi baadaye?
"Inapotokea hivyo hatufurahii sana tunaposhinda na tunapopoteza hatuchukulii kama jambo la ajabu sana. Ndiyo maana nadhani klabu iko imara."
Japo hali inaonekana kuwa sawa, lakini suala la Manchester United, kutokuwa na uhakika juu ya umiliki wa timu, malumbano ya hadharani kati ya meneja na wachezaji, ghasia za wafuasi na maswali juu ya ajira, vinaonyesha kuwa hali ya uthabiti ni jambo ambalo liko mbali na klabu hiyo.
Kwa hivyo, kama ilivyotokea wakati wa enzi za Louis van Gaal, Jose Mourinho na Ole Gunnar Solskjaer, maendeleo makubwa yaliyopatikana katika msimu mmoja chini ya Erik ten Hag yako katika hatari ya kurudi nyuma katika msimu ujao.
Uteuzi wa Ralf Rangnick kama meneja wa muda wakati Solskjaer alipofutwa kazi mnamo Novemba 2021 sasa unachukuliwa kuwa kosa.
Hata hivyo, Mjerumani huyo alipofika Old Trafford, moja ya vivutio vikuu wa maarifa yake makubwa aliyoyapata kupitia kazi yake kubwa kama mkurugenzi wa michezo katika kundi la Red Bull. Ujumbe ulikuwa kwamba utaalamu huu ungeweza kupatikana kwa United kwa miaka miwili ya ziada.
Rangnick alipata mafanikio dhahiri, tathmini yake ya kwanza kwa umma mnamo Machi 2022, kabla ya kushindwa kwa 4-1 na Manchester City.
"Kinachoonekana wazi, sio tu na Manchester City lakini pia na Liverpool, ni kwamba wamekuwa na mwendelezo na uthabiti na kocha wao mkuu, wana utambulisho wazi kabisa na wazo wazi la jinsi wanataka kucheza," alisema.
"Wazo hili ni kichwa cha habari kwa kila kitu kinachotokea katika klabu. Hii ndiyo siri ya mafanikio yao. Ni kile ambacho klabu zote za juu za Ulaya zinafanana. Ni jambo ambalo Manchester United inahitaji kuendeleza na kuboresha katika miaka michache ijayo."
Mwezi uliofuata, baada ya kushindwa 4-0 na Liverpool, Rangnick alisema:
“Huhitaji hata miwani kuona na kuchambua matatizo yalipo,” alieleza. "Haitoshi kufanya marekebisho madogo - mambo ya vipodozi. Katika dawa unaweza kusema kuwa hii ni operesheni ya kupasua moyo."
Tatizo kwa Rangnick ni kwamba sio kila mtu katika United alikubali upasuaji kama huo ufanyike.
United inazingatia 'mkataba rahisi'
Badala yake, walihisi ten Hag angeweza kutoa uboreshaji unaohitajika kupitia mpango wao wenyewe wa kuajiri. Wamempa £350m zaidi za kutekeleza hilo.
Lakini, kulingana na tathmini ya baadhi ya waangalizi , kuajiri kunaonekana kujikita katika kufanya mikataba 'rahisi'.
Kuwasili kwa Casemiro kutoka Real Madrid msimu uliopita kwa ada ya awali ya £60m kulipongezwa, lakini inafaa kukumbuka kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alianza msimu uliopita kwenye benchi ya Real.
Christian Eriksen pia aliingia kwa uhamisho huru, akichagua kujiunga na United badala ya kusaini mkataba wa muda mrefu na Brentford. Pia walilipa pauni milioni 13 kumsaini Tyrell Malacia kwa mkataba wa miaka minne kabla, hatimaye winga wa Brazil Antony alifika siku ya mwisho kwa pauni milioni 82, ukiwa ni usajili mkubwa wa pili katika historia ya klabu hiyo.
Je, mkataba wowote kati ya hii unaweza kuchukuliwa kuwa mgumu?
Ilikuwa vivyo hivyo kwa Rasmus Hojlund msimu huu wa joto - £72m liliwa ni ongezeko lmara tano ya jumla ya pesa iliyolipwa kwa Sturm Graz na Atalanta miezi 12 tu iliyopita.
United pia ililipa Chelsea £55m kumnunua Mason Mount, ambaye alikataa kusaini mkataba wa nyongeza na Stamford Bridge, ambako alikuwa amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake.
Andre Onana aliwagarimu pauni milioni 47.2 baada ya Ten Hag kuchukua uamuzi wa kijasiri wa kuachana na David de Gea, akiamini kuwa uwezo bora wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon akiwa na mpira miguuni mwake ungekuwa mzuri.
Na, wakati wengi wanahisi kiungo wa kati wa Uingereza Declan Rice angekuwa sawa kabisa na United, badala yake waliishia kumsajili Sofyan Amrabat, awali kwa mkopo, kutoka Fiorentina.
Sakata la Sancho na matatizo ya wachezaji
Kando na majeraha ya Luke Shaw, Lisandro Martinez, Casemiro na Aaron Wan-Bissaka, kulikuwa na mchezaji mwingine mmoja ambaye huduma zake hazikuzingatiwa na Ten Hag dhidi ya City.
Ingawa Jadon Sancho bado hajafanya mengi kuhalalisha malipo ya Solskjaer ya £73m aliyomlipa miaka miwili iliyopita, mvutano unaoendelea kati ya winga huyo wa Uingereza na Ten Hag hauleti sura nzuri kwa pande zote mbili.
Sancho ametiwa moyo na wachezaji wenzake kuwasilisha ombi la kuomba msamaha kwa Ten Hag kwa chapisho lake la uchochezi kwenye mtandao wa kijamii, ambalo lilikuja kujibu tamko la meneja wake kuwa alichapwa na Arsenal mnamo 3 Septemba kwa sababu ya mazoezi ya kiwango cha chini.
Wakati BBC Sport imeambiwa kuwa hali ya Sancho ni ngumu, ilielezwa kuwa masuala kama hayo yanashughulikiwa vyema kwenye uwanja wa mazoezi wakati yanapotokea.
Lakini maneno ya Sancho, ambayo sasa yamefutwa, yalikuwa ya kulaani na kulalamikia kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 kufanywa "mbuzi wa kafara". Je, inasadikika kuwa yeye ndiye mchezaji pekee anayehisi hivyo? Na hilo linaelezea nini kumhusu Ten Hag na namna ambavyo amekisimamia kikosi chake?
Ten Hag aliwasili kutoka Ajax karibu miezi 18 iliyopita, baada ya kujitengenezea sifa ya kocha wa kisasa aliyejitolea kwa mchezo mkali.
Aliiambia Viaplay baada ya kichapo cha 3-0 Jumapili dhidi ya City ya Guardiola kwamba kuwa na uwendani sawa na wa Ajax katika Old Trafford kwa sababu hana wachezaji na badala yake hitaji kuwa moja kwa moja.
Hata hivyo mchambuzi wa Mechi Bora ya Siku Danny Murphy si yeyey pekee katika kufikiria baadhi ya wachezaji walioimarika zaidi wa United hawana bidii ya kutosha.
Je, Sir Jim Ratcliffe anaweza kuweka alama yake?
Suala hili linahusu utafutaji unaoendelea wa United wa kutafuta "mkakati mbadala", uliozinduliwa tarehe 22 Novemba mwaka jana kwa lengo la "kuongeza ukuaji wa klabu, lengo kuu la kuweka klabu kuchangamkia fursa uwanjani na kibiashara" .
Kufuatia kujiondoa kwa Sheikh Jassim, ambaye alisisitiza kwamba azma yake ya kununuakwa 100% timu ya Manchester United ilikuwa bora zaidi kwa klabu, sasa inaonekana kuwa mzabuni mwingine mkuu, Ineos Group ya Sir Jim Ratcliffe, atachukua 25% ya awali ya hisa.
Ataingia katika klabu ambayo deni lake la jumla, likijumuisha ada ya uhamisho iliyosalia, sasa ni zaidi ya £1bn.
Imependekezwa Ratcliffe atakuwa na udhibiti wa masuala yote ya katika biashara ya ukubwa wa United, ambayo ni ngumu. Hata wale walio karibu na Ratcliffe wanawaza iwapo j mtu anayedhibiti mwenye umri wa miaka 71 ataweza kufanya kazi pamoja na familia ya Glazer, ambao wameendesha upande wa kibiashara wa klabu hiyo na hawakuwa na hofu ya kufanya maamuzi ambayo yanawanufaisha bila kujali ukosoaji wa nje. .
Ikiwa kifo cha Sir Bobby Charlton hakingechukua nafasi ya kwanza, ingekuwa rahisi kufikiria matarajio ya familia ya Glazer kubaki 'mamlakani' katika Old Trafford na kusababisha maandamano zaidi ya wafuasi.
Kwa kuzingatia matokeo ya mchezo wa Jumapili, ni jambo lisiloepukika kwamba hali ya wasiwasi ya mashabiki itaibuka tena hivi karibuni.
Miezi kumi na minane iliyopita, Rangnick aliwapa majibu. Lakini hakuna aliyesikiliza.