Kwa mara ya kwanza katika historia ya vilabu vya ligi kuu ya premia, EPL katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imechafuliwa na vilabu vya Manchester United na Newcastle Unite.
Hii ni baada ya vilabu hivyo viwili kumaliza mkiani mwa hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa na hivyo kubanduliwa nje hadi kukosa nafasi ya kushiriki kwenye ligi ya Uropa.
Katika historia ya vilabu vya EPL, hii ni mara ya kwanza vilabu vyake viwili vinamaliza mkiani mwa makundi ya michuano hiyo.
Kikosi cha Erik ten Hag kilishindwa 1-0 na Bayern Munich siku ya Jumanne, huku Newcastle ikipokea kichapo cha 2-1 kutoka kwa AC Milan siku moja baadaye.
Uchezaji mbaya wa vilabu hivyo barani Ulaya una madhara kwa Ligi Kuu. Hiyo ni kwa sababu Ligi ya Mabingwa inapanuliwa kutoka timu 32 hadi 36 msimu ujao, na ligi mbili zikipokea nafasi ya ziada. Nafasi zingine zimehifadhiwa kwa timu mbili bora katika viwango vya mgawo vya UEFA ambazo zilishindwa kufuzu kupitia njia ya kawaida.
Kwa hali ilivyo, Bundesliga (wastani wa 13.36) na Serie A (13.14) ndizo ligi mbili zitakazopokea nafasi ya ziada ya Ligi ya Mabingwa. Premier League ni ya tatu kwenye orodha hiyo (12.13) na itahitaji vilabu vyao kufanya vyema baada ya Krismasi ili kuruka ndani ya mbili bora.
Vilabu vyote 16 vinavyoshiriki katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa sasa vimethibitishwa. Bayern, Copenhagen, PSV, Real Madrid, Napoli, Real Sociedad, Inter Milan, Atletico Madrid, Lazio, Borussia Dortmund, Paris Saint-Germain, RB Leipzig, Barcelona na Porto zote zimepiga hatua. Arsenal na Manchester City watawakilisha Uingereza.