Aliyekuwa meneja wa timu ya taifa ya Uingereza Sven-Goran Eriksson amegundulika kuwa na saratani.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 75, ambaye aliiongoza Three Lions kati ya 2001 na 2006, alifichua kwamba ana 'angalau mwaka mmoja tu' wa kuishi, jarida la talkSPORT limebaini.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya kutamausha, Eriksson alikiambia kituo cha redio cha P1 cha Uswidi: "Kila mtu anaelewa kuwa nina ugonjwa ambao sio mzuri. Kila mtu amekuwa akisia kuwa ni saratani na ndivyo ilivyo. Lakini lazima nipigane kwa muda mrefu niwezavyo."
Alipoulizwa utabiri maalum, Msweden aliongeza: "Labda nikienda sana ni mwaka, mbaya zaidi ni miezi, au bora pengine nitaishi zaidi. Huwezi kuwa na uhakika kabisa. Ni bora usifikirie juu yake."
Eriksson alijiuzulu hivi majuzi kutoka wadhifa wake kama mkurugenzi wa michezo wa Karlstad katika asili yake ya Uswidi.
Alitafuta ushauri wa kimatibabu baada ya kuanguka wakati wa kukimbia kwa kilomita 5, na madaktari pia waligundua kuwa aliugua kiharusi.
Eriksson aliongeza: "Ona chanya katika mambo, usijisumbue katika shida, kwa sababu hii ndiyo shida kubwa bila shaka, lakini fanya kitu kizuri kutoka kwayo.
"Hawajui ni muda gani nilikuwa na saratani, labda mwezi au mwaka."
Meneja huyo wa zamani alichukua mikoba ya Roma, Benfica, Lazio, Manchester City na Mexico wakati wa kazi yake nzuri.
Eriksson alikusanya mataji 13 makubwa, akishinda Ligi Kuu ya Ureno mara tatu akiwa na Benfica na Serie A ya Italia mara mbili akiwa na Lazio.
Huko Uingereza, anajulikana sana kwa miaka mitano ya kuinoa timu ya taifa baada ya kuchukua mikoba ya Kevin Keegan mnamo 2001.