logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sancho avunja kimya baada ya kuondoka Man United kujiunga tena na Dortmund

Borrusia Dortmund ilibainisha kwamba winga huyo atasalia katika klabu hiyo hadi Juni 30, 2024.

image
na SAMUEL MAINA

Michezo11 January 2024 - 13:04

Muhtasari


  • •United ilithibitisha kwamba staa huyo mwenye umri wa miaka 23 amejiunga tena na klabu yake ya zamani, Borrusia Dortmund.
  • •Borrusia Dortmund ilibainisha kwamba winga huyo atasalia katika klabu hiyo hadi Juni 30, 2024.

Klabu ya soka ya Manchester United imethibitisha kuondoka kwa winga Jadon Sancho.

Katika taarifa ya Alhamisi mchana, klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza ilithibitisha kwamba staa huyo wa soka mwenye umri wa miaka 23 amejiunga tena na klabu yake ya zamani, Borrusia Dortmund.

Uhamisho wa Sancho hata hivyo sio wa kudumu kwani amejiunga tena na timu hiyo ya Ujerumani kwa mkopo hadi mwisho wa msimu wa EPL 2023/24.

"Sancho sasa atarejea Ujerumani kwa muda huku Borussia Dortmund wakijiandaa kuanza tena kampeni yao ya Bundesliga baada ya mapumziko ya msimu wa baridi. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza aliyecheza mechi za kimataifa 23 anaondoka na tunawatakia heri katika kipindi kilichosalia cha msimu huu,” Man United ilisema katika taarifa iliyotumwa kwenye tovuti yake rasmi.

Borrusia Dortmund pia ilithibitisha kurejea kwa winga huyo mwenye umri wa miaka 24 na kufichua kwamba atasalia katika klabu hiyo hadi Juni 30, 2024.

Wakati akitangaza kurejea kwake, mchezaji huyo alisema anajivunia sana kujiunga tena na klabu hiyo ya Ujerumani na kusema kwamba ana hamu ya kuicheza tena.

“Halo mashabiki wa BVB. Hapa ni kwa Jadon. Nataka tu kusema heri ya mwaka mpya. Nimefurahi sana kurejea na siwezi kusubiri kuanza. Ona uone na utunze,” Sancho alisema kwenye video aliyorekodi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved