Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2023) yanayoendelea nchini Ivory Coast yaliingia siku ya nne mnamo Jumanne, Januari 16, huku mechi tatu zikichezwa jioni
Mechi ya kwanza kati ya Burkina Faso na Mauritania ilishuhudia timu hizo mbili ambazo zilionekana kuwa na nguvu sawa zikichuana vikali hadi kukaribia kumaliza mchuano huo kwa sare kabla ya mshambuliaji wa Aston Villa Bertrand Traore kuifungia Burkina Faso bao la ushindi katika dakika ya 90+6.
Timu zote mbili zilikuwa zimekosa nafasi nyingi za kufunga katika mechi yote lakini Mauritania ilivunjwa moyo katika dakika za mwisho na kuwaachwa katika nafasi ya mwisho katika kundi D.
Namibia pia walipata ushindi wa kushtukiza wa 1-0 dhidi ya moja ya miamba ya soka wa Afrika Kaskazini, Tunisia baada ya kuonyesha mchezo mzuri katika mechi hiyo iliyochezwa saa mbili jioni.
Mshambulizi wa Orlando Pirates, Deon Hotto aliifungia Namibia bao la ushindi katika dakika ya 88 baada ya nchi hiyo ya Afrika Kusini kuwapa wakati mgumu wapinzani wao katika muda wote wa mechi.
Afrika Kusini ilipata kichapo kibaya cha mabao 2-0 dhidi ya Mali huku mabao yote mawili yakifungwa katika kipindi cha pili.
Mchezaji wa zamani wa Brighton, Percy Tau alikosa penalti katika kipindi cha kwanza kabla ya Hamari Traore na Lassine Sinayoko kuifungia Mali mabao mawili katika dakika ya 60 na 66 mfululizo.
Mashindano hayo sasa yanaingia siku ya tano mnamo Jumatano, Januari 16 huku mechi mbili pekee zikichezwa jioni.
Tazama ratiba ya mechi za Jumatano hapa chini;-
KUNDI F: Morocco vs Tanzania (Saa mbili usiku masaa ya Afrika Mashariki, katika uwanja wa Stade Laurent Pokou (San Pedro)
Kundi F: D.R Congo (Saa tano usiku masaa ya Afrika Mashariki, katika uwanja wa Stade Laurent Pokou (San Pedro)