logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Man United kumkosa Anthony Martial kwa kipindi kirefu kufuatia upasuaji mkubwa

Kulingana na Mashetani Wekundu, mwanasoka huyo alifanyiwa upasuaji huo mkubwa ili kurekebisha tatizo la kinena.

image
na Samuel Maina

Michezo24 January 2024 - 12:56

Muhtasari


  • •Kulingana na Mashetani Wekundu, mwanasoka huyo alifanyiwa upasuaji huo mkubwa ili kurekebisha tatizo la kinena.
Mshambulizi Anthony Martial

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Anthony Martial amefanyiwa upasuaji mkubwa wa kinena chake.

Habari za kufanyiwa upasuaji wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 zilitolewa na klabu hiyo ya EPL mnamo Jumatano alasiri kupitia tovuti yake rasmi.

Kulingana na Mashetani Wekundu, mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa alifanyiwa upasuaji huo mkubwa ili kurekebisha tatizo la kinena. Sasa atakuwa nje kwa zaidi ya miezi miwili.

"Mshambulizi wa Manchester United Anthony Martial amekamilisha upasuaji uliofaulu kushughulikia matatizo yake ya kinena na atakuwa nje ya uwanja kwa takriban wiki 10 atakaporejea," ilisema taarifa ya Man United.

Waliongeza, "Tunamtakia Anthony apone haraka na tunatazamia kurejea kwake."

Wiki iliyopita, vyombo vya habari vya Uingereza vilifichua kwamba mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 aliambiwa afanye mazoezi peke yake ili kuboresha hali yake kabla ya kuchaguliwa tena na meneja Erik ten Hag.

Martial hata hivyo amekuwa akilalamika kuhusu suala la paja, ambalo United wamethibitisha kuwa amefanyiwa upasuaji katika jitihada za kutatua suala hilo. Huenda asipatikane hadi mwanzoni mwa Aprili.                                                

Hata hivyo, huku mkataba wake ukielekea kumalizika mwishoni mwa msimu huu, na tayari Mfaransa huyo akiwa tayari ameanza kutengwa kwenye kikosi hicho, kuna uwezekano mkubwa kwamba ameichezea klabu hiyo mechi yake ya mwisho.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved