Nahodha wa timu ya Taifa Stars nchini Tanzania, Mbwana Samatta amemtaja kocha wao aliyesimamishwa kazi, Adel Amrouche, kuwa ni “mmoja wetu” na kusema anatamani kikosi hicho kingekuwa naye kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 inayoendelea nchini Ivory Coast.
Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) lilimuadhibu Amrouche siku ya Ijumaa baada ya kufungiwa mechi nane na kutozwa faini ya dola 10,000 (pauni 7,900) na Shirikisho la Soka Afrika (Caf).
Hii inafuatia malalamishi kutoka kwa shirikisho la Morocco (RMFF) kwa Caf kuhusu matamshi yaliyotolewa na Amrouche.
"Yeye (Amrouche) alitutayarisha kuja Afcon na baada ya mchezo wa kwanza, alifungiwa.
Kwa hivyo ni ngumu kwa kundi," Samatta aliiambia BBC Sport Africa."Tunatamani tungekuwa naye.
Lakini hiki ndicho kilichotokea na hatuwezi kubadili hilo ili tukae pamoja.
"TFF imesema maoni ya Amrouche aliyoyatoa kabla ya Afcon kuanza, yamekosoa ushawishi wa RMFF kwenye mchezo wa Afrika.
Morocco tayari walikuwa wameifunga Tanzania 3-0 katika mechi yao ya ufunguzi ya Kundi F Jumatano iliyopita wakati Amrouche alipotangaza kusimamishwa.
Hemed Suleiman alikuwa kwenye dimba la Taifa Stars katika mchezo wake wa pili, sare ya 1-1 na Zambia Jumapili, na kocha huyo wa muda pia alimuunga mkono Amrouche.
"Tuna mshikamano kama makocha. Mnafanya kazi pamoja na ilikuwa ni dhamira yetu kuja kufanya kitu katika Afcon hii," alisema.
Tanzania, iliyo mkiani katika Kundi F ikiwa na pointi moja, inahitaji ushindi dhidi ya DR Congo katika mchezo wao wa mwisho wa kundi Jumatano (20:00 GMT) ili kujiwekea nafasi yoyote ya kutinga hatua ya 16 bora.
Samatta anasema pamoja na kukosekana kwa Amrouche, bado ni sehemu kubwa ya maandalizi ya timu hiyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 55 aliteuliwa kuwa kocha wa Tanzania Machi mwaka jana, akiwaongoza Waafrika Mashariki kufuzu Afcon kwa kupata pointi moja katika nchi yake ya kuzaliwa ya Algeria katika mechi yao ya mwisho ya kufuzu.
"Tulifanikiwa kucheza mchezo wetu dhidi ya Zambia na haikutuvunja moyo," mshambuliaji wa zamani wa Aston Villa Samatta aliongeza."
Tutajaribu kuhakikisha kwamba tunacheza mchezo wetu na kujaribu kushinda mchezo wetu.
Bado tunamfikiria kuwa pamoja nasi kwa sababu hatuwezi kumwacha atoke nje ya timu yetu. Yeye ni mmoja wetu."