Kocha Thomas Tuchel ataondoka katika klabu ya Bayern Munich mwishoni mwa msimu.
Tuchel mwenye umri wa miaka 50 alichukua nafasi ya Julian Nagelsmann katika klabu hiyo ya Ujurumani mwezi Machi 2023 katika mkataba uliokuwa umalizike Juni 2025.
Lakini mkufunzi huyo wa zamani wa Chelsea ataondoka mwaka mmoja kabla ya ilivyopangwa kama sehemu ya "mabadiliko ya michezo" huko Bayern.
Aliongoza Bayern msimu uliyopita kuchukua taji la Bundesliga baada ya kuchukua usukani majira ya machipuko lakini sasa wako alama nane nyuma viongozi Leverkusen baada ya kushindwa.
Mojawapo ya hizo ni kupoteza kwa 3-0 kutoka kwa Leverkusen- na pia walichapwa 1-0 na Lazio katika mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bayern Jan-Christian Dreesen alisema pande zote mbili zilikubaliana "kumaliza ushirikiano wetu" kufuatia "mazungumzo ya wazi na mazuri".
"Lengo letu ni kufanya maelewano ya kimichezo na kocha mpya kwa msimu wa 2024-25," aliongeza.
"Hadi wakati huo, kila mtu katika klabu ana changamoto kubwa ya kufikia kiwango cha juu iwezekanavyo katika Ligi ya Mabingwa na Bundesliga.
"Pia ninawajibisha timu kwa uwazi. Hasa katika Ligi ya Mabingwa, tuna hakika baada ya kushindwa huko Lazio tutatinga robo fainali huku mashabiki wetu wakiwa nyuma yetu."
Tuchel, ambaye pia amewahi kuinoa Paris St-Germain na Borussia Dortmund, alisema: "Tutaondoka baada ya msimu huu.
Hadi wakati huo, mimi na timu yangu ya ukufunzi tutaendelea kufanya kila tuwezalo kuhakikisha tunapata mafanikio ya hali ya juu."