Dakika chache baada ya kipenga cha mwisho katika ngarambe ya Chelsea dhidi ya Liverpool kwenye fainali ya Carabao, Manchester City walichukua kwenye ukurasa wa X kumpiga kijembe aliyekuwa kinda wao Cole Palmer ambaye anaiwajibikia The Blues.
Cole Palmer ambaye aliondoka Manchester City kishari kwa kunyimwa muda wa kutosha uwanjani na meneja Pep Guardiola alishindwa kuisaidia Chelsea kutwaa taji hilo ambalo liliwaponyoka kunako dakika ya 118 kufuatia mpira wa kichwa maridadi kutoka kwa nahodha wa Liverpool Van Dijk uliotua wavuni.
City walielekea katika ukurasa wa X na kuweka picha na kinda wao mwingine waliyekuwa waking’ang’ania namba na Palmer, Phil Foden na kuweka emoji za ‘cold’ – kuashiria jinsi ambavyo Palmer anapenda kusherehekea pindi anapofunga bao.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ana mabao kumi na asisti sita katika Premier League msimu huu - hakuna mchezaji wa Chelsea aliye na zaidi. Amekutana na timu yake ya zamani mara mbili, akifunga penalti ya dakika za lala salama Stamford Bridge mwaka jana na kuokoa pointi.
Amekuwa maarufu kwa mbinu yake ya kusherehekea ‘cold’.