Mchezaji wa Super Eagles wa Nigeria na klabu ya Atalanta Ademola Lookman amefunguka jinsi alipata kujifunza mengi kisoka kutoka kwa Sadio Mane, aliyekuwa winga wa Liverpool na timu ya taifa ya Senegal.
Lookman, ambaye alisifiwa kwa uchezaji wake wa kuvutia katika Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Januari, anasema ujuzi wa soka wa Mane unampa mawazo mengi.
"Mvulana ambaye siku zote nikimtazama sana angekuwa Sadio Mane.”
“Nikiangalia tishio lake kwenye eneo la hatari, tishio lake katika nafasi hizo ndogo ndogo, mwendo wake—nimetazama sana mchezo wake hasa,” Lookman aliambia jarida la udaku la The Athletic.
Tangu mchezo wake wa kuvutia katika mashindano ya AFCON, Lookman anasema anaona soka katika hali mpya.
"Ninahisi kama ninaelewa soka zaidi sasa. Hapo awali, sikuwahi kuona soka jinsi ninavyoiona sasa. Ninapotazama michezo, mimi hutafuta vitu fulani kulingana na miondoko na nafasi - maelezo hayo madogo ambayo sikuwahi kuyatafuta hapo awali," Lookman anafichua.
Lookman alijiunga na klabu ya Serie A ya Atalanta kwa mkataba wa miaka minne kwa ada iliyoripotiwa ya Euro milioni 15 mnamo Agosti 4, 2022.