logo

NOW ON AIR

Listen in Live

The Blues wanyolewa kichwa bila maji ugani Emirates

Ushindi wa Jumanne jioni uliwapeleka vijana wa Mikel Arteta kileleni mwa jedwali wakiwa na pointi 77.

image
na Samuel Maina

Michezo24 April 2024 - 04:53

Muhtasari


  • •Vijana wa Mauricio Pochettino walishindwa kufunga bao lolote huku wapinzani wao wa usiku wa Jumanne wakifunga mabao matano.
  • •Ushindi wa Jumanne jioni uliwapeleka vijana wa Mikel Arteta kileleni mwa jedwali wakiwa na pointi 77 na pia kuboresha tofauti yao ya mabao.

Klabu ya soka ya Chelsea ilipata kichapo kikubwa na chungu kutoka kwa wapinzani wao wakubwa Arsenal katika mechi ya kusisimua iliyochezwa kwenye Uwanja wa Emirates jijini London, Uingereza siku ya Jumanne usiku.

Vijana wa Mauricio Pochettino walishindwa kufunga bao lolote huku wapinzani wao wa usiku wa Jumanne wakifunga mabao matano dhidi ya kipa Djordje Petrovic.

Mchezaji wa Kimataifa wa Ubelgiji Leandro Trossard alifunga bao la kwanza la  Wanabunduki dakika nne tu baada ya mchuano kuanza.

Timu zote zilipata nafasi kadhaa za kufunga katika dakika zilizosalia za kipindi cha kwanza lakini hakuna hata mmoja wao aliyebadilisha nafasi hizo kuwa mabao.

Ilikuwa ni kipindi cha pili ambapo Wanabunduki walionyesha ukali wa risasi zao huku wakifunga mabao manne zaidi na kuwashinda majirani zao jijini London.

Mshambulizi wa zamani wa Chelsea, Kai Harvetz na beki wa kulia wa Uingereza, Ben White walifunga mabao mawili kila mmoja na kuipa Arsenal ushindi muhimu wakati wanapigania kombe la EPL 2023/34 na Manchester City na Liverpool.

Ushindi wa Jumanne jioni uliwapeleka vijana wa Mikel Arteta kileleni mwa jedwali wakiwa na pointi 77 na pia kuboresha tofauti yao ya mabao.

Manchester City hata hivyo wana michuano miwili ambayo hawajacheza ambayo inaweza kuwapeleka kileleni mwa jedwali iwapo watashinda.

 Kwa upande wao, Liverpool wana mchuano mmoja ambao haujachezwa na ushindi utawafanya wao na Arsenal kuwa sawa kwa pointi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved