Mshambulizi wa klabu ya West ham yenye makaazi jijini London na raia wa Jamaica, Michael Antonio ameelezea maoni yake kuhusu ni nani atakayenyakua taji kuu la primia msimu huu iwapo mechi ya mwisho itaamua baina ya wapambanaji wawili.
Kwenye majadiliano kati yake na wachapishaji wa gazeti la 'The Footballer's Football ', Antonio amesema kuwa Arsenal wana uwezo wa kunyakua taji hilo kwa kuwa West Ham wapo katika harakati ya kuwania mashindano ya bara ulaya .
'Mechi ya mwisho ya msimu huu, sisi [West Ham ]tuna kitu cha kuchezea pia,tunajaribu kuingia ulaya...'
West Ham watachuana na Manchester City kwenye mechi ya mwisho ya msimu jumapili 19. Iwapo wataibuka na ushindi nayo Arsenal iwanyoroshe Everton , basi maneno yake Michael Antonio yatakwenda sawa .Arsenal itakuwa mbele ya manchester city kwa alama moja,hivo kutawazwa mabingwa.
Kwa sasa West Ham wanashikilia nafasi ya tisa kwa alama 52, na iwapo chelsea na manchester united watakosa kushinda mechi zao , basi West Ham watakuwa wataajikatia tiketi ndani ya mashindano ya bara Ulaya.
Je , Manchester City watapokonywa taji na wanabunduki, Arsenal ?