logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Man U yataja wachezaji 4 ambao haitawauza liwe liwalo; Mainoo, Onana, Hojlund na Garnacho

United wako tayari kusikiliza ofa kwa wachezaji wote isipokuwa wanne.

image
na Davis Ojiambo

Michezo29 May 2024 - 09:55

Muhtasari


  • • Bosi wa sasa Erik ten Hag tayari anakabiliwa na mustakabali usio na uhakika Old Trafford, na ripoti zikipendekeza anaweza kuonyeshwa mlang

Huku kukiwa na ripoti kuhusu klabu ya Manchester United kusafisha kikosi chao kwa kuwaachilia wachezaji karibia wote katika kikosi cha sasa cha kwanza, ripoti mpya zimeibuka kuhusu baadhi ya wachezaji ambao uongozi wa klabu hiyo umeapa katu kutowaachilia kwa gharama yoyote ile.

Mmiliki mpya mwenye hisa chache, Jim Ratcliffe anadokezwa kufanya mabadiliko makubwa katika klabu hiyo, ikiwemo ni pamoja na kutafuta wachezaji nguvu mpya weney ari ya kuitumikia klabu kwa ajili ya kurejea katika mkondo wao wa zamani wa kushinda mataji.

Kulingana na SPORTbible, licha ya United kumaliza kampeni yao mbaya na Kombe la FA, mabadiliko makubwa yanatarajiwa katika idara zote.

Bosi wa sasa Erik ten Hag tayari anakabiliwa na mustakabali usio na uhakika Old Trafford, na ripoti zikipendekeza anaweza kuonyeshwa mlango.

Kikosi kinachocheza kinadaiwa kukabiliwa na hali kama hiyo, huku wachezaji wengi wakiwa katika hatari ya kuhamishwa.

Kiasi kwamba Telegraph hivi majuzi ilidai kwamba wakuu wa United wako tayari kusikiliza ofa kwa wachezaji wote isipokuwa wanne.

Kulingana na ripoti, Alejandro Garnacho, Kobbie Mainoo, Andre Onana na Rasmus Hojlund hawamo kwenye ubao wa kutemwa nje.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved