Mshambulizi hodari wa Harambee Stars ambaye pia ni nahodha wa kikosi hicho Michael Olunga, anaamini anaweza kutumia umahiri wake katika kuipeleka Kenya kwenye mashindano ya ubingwa wa kombe la dunia.
Olunga anayeichezea timu ya Al Duhail SC kwenye ligi kuu nchini Qatar alizungumza baada kumaliza kama mwafrika wa tano aliye na mabao zaidi katika ligi za ughaibuni.
Olunga alijinyakulia nafasi hiyo nyuma ya Sadio Mane aliye na mabao ishirini na matano akifuatiwa na kiungo Serhiu Guirassy wa Guinea na mabao thelathini na mmoja kisha kufutwa mchezaji mashuhuri Pierre Emerick Aubamayeng wa Gabon aliyenyakua nafasi ya tatu kwa mabao thelathini.
Kiungo mahiri wa Morocco na Al Ittihad Abderazak Hamdallah alikuwa wa nne na mabao ishirini na tisa kisha kufuatiwa naye Michael Olunga aliyenyakua mabao ishirini na manane msimu huu.
"Ninayo mabao kwenye wahitimu na nitatumia uzoefu huu kuwinda mabao zaidi katika mechi zinazokuja hivi karibuni,” alisema Olunga.
Hata hivyo, Olunga alisikitika kwa kuwa mechi za nyumbani zilipelekwa kuchezwa kwenye uga wa nchi ya Malawi mjini Lilongwe kufuatia agizo la FIFA la kuwa na viwanja murua vya kuchezea.
“Mashabiki wana jukumu azizi kwenye matokeo ya timu. Mfano, Gabon walitucharaza 2-1 kupitia nguvu za mashabiki wao wakati tulicheza kwenye uga wao,” aliongezea.
Mechi za mwisho walizocheza Harambee Stars waliibuka washindi kwenye mashindano ya nchi nne ambapo waliwacharaza wenyeji Malawi mabao manne kwa bila kisha kuwanyorosha Zimbabwe tatu kwa moja kwenye fainali na kuibuka mabingwa.