logo

NOW ON AIR

Listen in Live

VAR kuendelea kutumika katika ligi kuu ya Uingereza (EPL)

Vilabu vya ligi kuu ya Uingereza vimepiga kura kupitisha kuwepo kwa VAR hii ni baada ya Wolves kuwasilisha malalamishi.

image
na Davis Ojiambo

Michezo06 June 2024 - 14:10

Muhtasari


  • •Vilabu vya ligi kuu ya Uingereza vimepiga kura na kuidhinisha VAR kusalia japo marekebisho kidogo yafaa kuangaziwa
  • •Wolves walianzisha hoja ya VAR kuondolewa baada ya msururu wa maamuzi ya VAR kuwakandamiza msimu uliopita.
VAR

Vilabu vingi vimeonyesha nia ya kuona maboresho yakifanywa kwa mchakato wa VAR, badala ya kuondolewa kabisa kwa teknolojia hiyo.

Wolves walikuwa wameongoza msukumo wa kufuta mfumo huo baada ya msururu wa makosa, lakini katika kura ya Alhamisi, uamuzi ulifanywa  huku kura ikionyesha kutofutiliwa mbali kwa VAR.

"Kama sehemu ya majadiliano ya kina katika mkutano mkuu wa mwaka, ilikubaliwa kuwa PGMOL, Ligi Kuu na vilabu vyote vina majukumu muhimu ya kutekeleza...:' Taarifa ilisema.

Ligi ya Premia imekuwa kwenye shinikizo kubwa la kutaka kurekebisha VAR, ambayo ilianzishwa mwanzoni mwa msimu wa 2019.

Aidha ,2024 kutakuwa na utekelezaji wa teknolojia ya kuotea ya nusu otomatiki, ambayo imeundwa ili kuharakisha mchakato wa VAR na kupunguza uwezekano wa makosa.

Pia kuna mipango ya utangazaji wa moja kwa moja wa video na sauti za maamuzi ya VAR ili kuhakikisha watazamaji wanafahamishwa kuhusu michakato inayoendelea.

Matangazo ya ndani ya mchezo, ambayo yalitumika wakati wa Kombe la Dunia la wanawake 2023, yatawaruhusu waamuzi kuelezea maamuzi ya baada ya VAR kwa wafuasi kwenye viwanja.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved