Chelsea wapo kwenye mazungumzo ya juu ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa na Colombia Jhon Duran, kulingana na ripoti kutoka majarida ya spoti.
The Blues wamekuwa wakisaka mshambuliaji, baada ya kuhusishwa kwanza na Victor Osimhen, kisha Benjamin Sesko, ambaye ameamua kusalia Ujerumani, kabla ya kurejea tena kutaka kumnunua Duran kutoka Villa.
Gazeti la En La Jugada linaripoti kuwa,Chelsea wana makubaliano na Villa kwa ajili ya Duran kwa zaidi ya mara mbili ya bei waliyolipa kutoka MLS, na mkataba huo unakaribia kufikia pauni milioni 40.
Msimu uliopita ,Chelsea walimtaka mshambuliaji huyo wa Colombia lakini wakaachana na nia yao na kuelekeza nguvu zao kwa Sesko ambaye kwa sasa amesaini mkataba mwingine na RB Leipzig.Uamuzi wa mchezaji huyo,umeifanya Chelsea kuharakisha mazungumzo na Villa ili kumpata Duran.
Licha ya kuwa mbadala wa Ollie Watkins, Duran alifunga mabao matano ya ligi, nane kwa jumla ukiongeza mechi za ligi ya Europa.
Mwezi uliopita, ajenti wa Duran, Jonathan Herrera alidokeza kwamba mchezaji huyo anaweza kuondoka baada ya kukiri kuwa mchezaji huyo hapati muda mwingi wa kucheza. Aliiambia El VBar Caracol ya Colombia:
"Ni mchezaji ambaye ana mkataba na Aston Villa, aliishia kufanya vizuri sana, na kocha anamtegemea. Ni klabu ambayo, baada ya kuingia kwenye ligi ya mabingwa, ndiyo. nafasi nzuri, lakini tunajua anataka kucheza, anataka kuonekana akicheza..."
Aliongezea kuwa Chelsea imeonyesha ari ya kumchukua raia huyo wa Colombia,na kwa sasa klabu ipo tayari kuskiza.
"Sasa soko linafunguliwa, klabu inaangalia baadhi ya chaguzi, na sisi pia. Nia [kutoka kwa Chelsea] imekuwepo kila wakati. Ukweli kwamba Pochettino anaendelea au anaondoka kwenye kilabu [haipaswi kuathiri]. anayemtaka mwishowe ni klabu....ni mchezaji ambaye, kama watabadilisha kocha au la yuko sawa, tutaona kitakachotokea, lakini kumekuwa na nia. Wacha tuone jinsi ya kushughulikia na kuhakikisha kuwa Aston Villa iko tayari."