Ratiba ya msimu mpya wa mwaka 2024/25 kwenye ligi kuu ya Premia nchini Uingereza imetolewa rasmi.
Ligi hiyo itang’oa nanga Ijumaa ya Agosti 16 ambapo Manchester United watawakaribisha Fulham ugani Old Trafford.
Wikendi ya kwanza ya msimu ambayo itakuwa Jumamosi ya Agosti 17 itashuhudia mechi ya mapema mwendo wa saa tisa mchana kati ya malimbukeni Ipswich wakiwakaribisha Liverpool.
Mechi zingine kwenye Jumamosi hiyo zitakuwa ni Arsenal dhidi ya Wolves, Everton dhidi ya Brighton, Newcastle dhidi ya Southampton, Nottingham Forest dhidi ya Bournemouth na Westham dhidi ya Aston Villa kufunga siku.
Jumapili ya kwanza ya msimu itashuhudia mechi kubwa ambapo Chelsea watakaribisha mabingwa watetezi Manchester City gani Stamford Bridge.
Jumatatu ya Agosti 19, malimbukeni Leicester City watamaliza udhia dhidi ya Tottenham Hotspurs.
Hii hapa ratiba kamili ya msimu mpya’