Uhispania walitinga hatua ya robo fainali na wenyeji wa michuano ya Euro 2024 Ujerumani kwa kunusurika na hofu ya mapema ya kuondolewa na Georgia baada ya kwa kupata ushindi wa maao 4-1.
Wakicheza katika mchuano wao wa kwanza muhimu, Georgia ililazimika kupata presha kubwa kutoka kwa Uhispania mapema lakini ikawashangaza wengi katika Uwanja wa Cologne walipopata uongozi wa kushtukiza baada ya dakika 18.
Beki wa Uhispania Robin le Normand alichombeza krosi ya Otar Kakabadze kwenye lango lake, akimalizia shambulizi la kushtukiza na kuwanyamazisha mashabiki nyuma ya lango lao.
Wachezaji wa akiba waliokuwa wakipasha misuli motowalimkimbilia Khvicha Kvaratskhelia, ambaye aliongoza sherehe za Georgia kwenye kona.
Jude Bellingham alionyesha kipaji cha kipekee baada ya kuiokoa England kwa kuwabakiza katika katika Euro 2024 baada ya hofu ya kuyaaga mashindano hayo alipofunga bao ambalo liliwapa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Slovakia kwa mtindo wa ajabu na kutinga hatua ya nane bora.
England walikuwa wamesalia sekunde chache kuyaaga mashindano hayo huku Slovakia wakilinda bao lao la kuongoza ambalo walikuwa wameshikilia tangu dakika ya 25 pale Ivan Schranz alipoingia kwenye eneo la hatari na kumshinda kipa wa Uingereza Jordan Pickford.
Hapo ndipo Bellingham, ambaye alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya mwaka wa 21 siku ya Jumamosi, alionyesha umahiri wake ambao umemfanya kuwa supastaa mpya wa England kwa kupaa angani katika eneo la hatari kuusuka vyema mpira wa kichwa wa Marc Guehi kumpita Martin Dubravka kwa kiki ya ajabu