Timu ya taifa ya kandanda ya Kenya Harambee Stars imewatambua wapinzani wao kwa mechi zijazo za kufuzu AFCON 2025
Droo hio ilifanyika nchini Afrika Kusini Julai 4 ,2024 kwa usaidizi wa kocha wa Ivory Coast,Emerse Fae na gwiji wa soka wa Morocco ,Marouane Chamakh .Mechi hizo zitafanyika kuanzia Septemba mosi hadi Novemba mwaka huu.
Kenya itakuwa mbioni kujaribu kufuzu kwa michuano hio kwa mara ya saba, baada ya kukosa kufuzu kwa makala ya 2023 kutokana na marufuku ya mwaka mzima waliyowekewa na FIFA mwaka wa 2022.
Kenya wamepangwa Kundi J, ambapo watakuwa wakicheza dhidi ya Zimbabwe, Namibia na Cameroon lengo lao likiwa ni kufuzu kwa mara ya kwanza tangu 2019.
Sadfa iliyoje,kwani Kenya iliwekwa pamoja na Cameroon katika mechi za kufuzu 2023 lakini haikukabiliana nayo kutokana na kupigwa marufuku, na hivyo itakuwa na nafasi ya kukabiliana nao tena.
Kenya imekabiliana na Zimbabwe mara mbili mwaka huu, na kuibuka washindi mara zote mbili. Pia watakuwa na matumaini ya kurekebisha makosa ya mechi ya kufuzu AFCON 2013 dhidi ya Namibia, ambapo hawakuweza kuwafunga nyumbani na ugenini.
Afcon 2025 itakuwa inaanza Disemba 21 na kukamilika Januari 18, 2025.
Hii hapa ni orodha kamili:
Kundi A:Tunisia,Madagascar, Comoros,Gambia
Kundi B:Morocco, Gabon ,Central Africa Republic, Lesotho
Kundi C :Egypt ,Cape Verde, Mauritania ,Botswana
Kundi D:Nigeria ,Benin, Libya ,Rwanda
Kundi E :Algeria, Equatorial ,Guinea,Togo,Liberia
Kundi F: Ghana ,Angola,Sudan ,Nigeria
kundi G: Ivory Coast, Zambia ,Sierra Leone, Chad
Kundi H :DR Congo, Guinea,Tanzania, Ethiopia
Kundi I: Mali ,Mozambique ,Ginea Bissau, Eswatini
Kundi J :Cmeroon, Namibia ,Kenya ,Zimbabwe
Kundi K :South Africa ,Uganda, Congo ,South Sudan
Kundi L:Senegal, Burkina Faso, Malawi ,Burundi