Timu ya taifa ya kandanda ya Kenya ya U23, Emerging Stars katika Kombe la COSAFA 2024 ilifikia kikomo, licha ya kumaliza nafasi ya pili katika Kundi B.
Matokeo haya yalifuatia kufuzu kwa Namibia na Angola kwa nusu fainali, huku timu zote zikimaliza kileleni mwa msimamo wa kundi.
Mozambique na Comoros tayari walikuwa wamefuzu kwenye nusu fainali.
Kenya ilimaliza ikiwa na pointi sita, sawa na vinara Comoro ambao walikuwa na tofauti ya mabao ya juu zaidi, na walikuwa wakipigania Angola na Namibia kutoka sare au kupoteza mechi zao za mwisho za Kundi C na kutinga nusu fainali.
Hata hivyo, Angola iliizaba Lesotho 3-1 na kumaliza kileleni mwa kundi hilo ikiwa na pointi saba, huku Namibia ikiishinda Seychelles na kumaliza nafasi ya pili baada ya mechi za Jumatano.
Namibia ilifuzu kwa nusu-fainali iliyopangwa Ijumaa, Julai 5, 2024, kama mshindi wa pili katika makundi yote matatu, ikitoa Kenya na Afrika Kusini.
Kenya walishinda Zimbabwe na Zambia katika kundi B, huku wakipoteza mechi mmoja pekee dhidi ya Comoro.
Katika nusu fainali, Comoro itamenyana na Angola katika mchezo wa kwanza, kabla ya Msumbiji kumenyana na Namibia katika mchezo wa pili.
Kenya ilikuwa miongoni mwa timu zilizoalikwa katika Kombe la COSAFA, lililoshirikisha timu 12. Muundo wa mashindano hayo uliruhusu washindi watatu wa makundi na timu bora iliyoshika nafasi ya pili kutinga nusu fainali.