Kikosi kamili cha wachezaji 29 cha United kilifanya mazoezi kwenye jua katika chuo cha UCLA huko California kwa ziara yao ya Marekani.
Huku wakurugenzi wapya Dan Ashworth na Jason Wilcox wakitazama pembeni kuona maendeleo ya klabu.
Mashabiki waliona kuwa zoezi moja lilivutia macho yao, na hivyo kupelekea mawazo yao kukimbilia kwenye uwezekano wa kampeni yao ya kushinda ubingwa. wa ligi kuu ya Uingereza.
Video hiyo iliyosambaa mtandaoni ilionyesha wachezaji wa United wakifanya zoezi linalofahamika kama 'Rondo'.
Mazoezi ya Rondo ni zoezi maarufu katika soka linalotumika kukuza ujuzi wa kiufundi wa wachezaji,kufanya maamuzi haraka ,na kazi ya pamoja.Zoezi hili husaidia kuboresha usahihi wa kupiga pasi,kudhibiti mpira,na kupunguza shinikizo kutoka kwa mpinzani.
Hata hivyo mashabiki hawakusita kuelezea furaha na maoni yao kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutazama video hio.
Mmoja aliandika: "United itakuwa mojawapo ya timu ya kupigiwa mfano msimu ujao."
Wakati mwingine aliongeza: "Hii ni ajabu".
Wa tatu alisema: "Tunashinda ligi!"