Klabu ya Manchester United inatarajiwa kufanya uamuzi mwishoni mwa mwaka iwapo itajenga uwanja mpya au kufanya ukarabati wa uga wa sasa,Old Trafford.
Kulingana na Sun football ,United wanapanga kutoa tangazo mnamo Disemba kuhusu uwanja huo mpya ambao utakuwa na uwezo wa kubeba watu 100,000 na kukamilika ifikapo 2030.
Klabu hiyo imekuwa katika harakati za kuchunguza baadhi ya viwanja vingine, vikiwemo Bernabeu ( uwanja wa klabu ya Real Madrid ) na Nou Camp ( uwanja wa klabu ya Barcelona) ambavyo vyote vimefanyiwa ukarabati mkubwa.
Viongozi wa klabu hio pia wamekuwa katika harakati ya kuchunguza uwanja wa SoFi uliopo Los Angeles kule Marekani ambapo United walicheza na Arsenal,Julai 28,2024.
Uwanja huo ulikamilika mwaka wa 2020 na ulikuwa sehemu ya ‘Hollywood Complex’ ya £4bn kutengeneza upya eneo kubwa la Inglewood.
Zote zilifadhiliwa na mmiliki wa Arsenal, Stan Kroenke na uwanja huo unaoweza kumiliki mashabiki takriban70,000 utaandaa michezo sita ya kombe la dunia 2026 ikiwa ni pamoja na ufunguzi wa shindano hilo.
United wanatazamia sio tu kujenga uwanja lakini kutengeneza upya eneo la Trafford ambapo uwanja utasimama.
Hata hivyo,wamiliki wa Man united wanakisia kuwa klabu yenye hadhi kama united inapaswa kuwa na kituo kipya cha hali ya juu.
Wanajali kudumisha utambulisho wa klabu katika uwanja mpya, ambao utajengwa kwenye ardhi karibu na makazi ya sasa ya Mashetani Wekundu hao.Old Trafford imekuwa nyumbani kwa United tangu 1910.
Klabu imeshauriana na mashabiki 30,000 kuhusu nini cha kufanya na inaamini kuna takriban mgawanyiko wa 50-50 wa kubaki au kuhamia uga mpya.
Ufadhili wa mradi huo bado unajadiliwa, kwa wazo la mchanganyiko wa ufadhili wa umma na wa kibinafsi.
United tayari imewasiliana na waziri mkuu mpya wa Leba, Keir Starmer, ambaye anasemekana yuko wazi kwa usaidizi wa serikali kwa viungo vya usafiri kama sehemu ya mradi huo.