Siku ya Jumatatu, Saudi Arabia iliwasilisha rasmi stakabadhi zake za kuhusu nia yake ya kugombea kuandaa Kombe la Dunia la 2034 katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, katika hafla iliyofanywa na Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA).
Stakabadhi hizo zilikabidhiwa na ujumbe rasmi ulioongozwa na Mwanamfalme Abdulaziz bin Turki bin Faisal, Waziri wa Michezo, Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki na Walemavu ya Saudia, na Rais wa Shirikisho la Soka la Saudia, Yasser Al-Meshal, pamoja na watoto wawili kutoka vituo vya mafunzo vya kikanda vya Chama cha Soka cha Saudi Arabia.
Waziri wa Michezo wa Saudia alisema: "Stakabadhi za Ufalme za kugombea kuandaa Kombe la Dunia la 2034 zinanajumuisha maono ya kina na ya wazi ya taifa hili kuu kuelekea mustakabali mzuri - Mungu akipenda."
Aliongeza: "Ufalme una nia ya kuandaa tukio muhimu zaidi katika ulimwengu wa soka, na hivyo kuthibitisha nafasi yake kubwa, yenye ushawishi na chanya kwenye ramani ya dunia nzima, katika nyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na michezo."