logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nahodha wa Harambee Starlets U20 Jane Hato yuko salama

Nahodha Jane Hato huenda akajiunga na wachezaji wenza Uhabeshi.

image
na Davis Ojiambo

Michezo16 August 2024 - 11:39

Muhtasari


  • •Shirikisho la soka nchini FKF nchini siku ya Alhamisi lilikuwa limeripoti kutoweka kwake, lakni sasa inasemekana amepatikana  na ataunganishwa na familia yake. 
JANE HATO

Nahodha wa timu ya kinadada ya Kenya isiyozidi umri nwa miaka 20 na kenya police Bullets Jane Hato yuko salama.

Shirikisho la soka nchini FKF nchini siku ya Alhamisi lilikuwa limeripoti kutoweka kwake, lakni sasa inasemekana amepatikana  na ataunganishwa na familia yake. 

Chris Oguso afisa mkuu mtendaji wa Kenya Police Bullets alisema kwamba Hato yuko salama na walitumia kila mbinu kuhakisha kwamba wamepata taarifa kuhusiana na kupotea kwake. 

"Sidhani kama haya ni maswala yanayofungamana na kandanda ila huenda ikawa ni mgogoro wa kifamilia ,na washikadau wetu wanazidi kutatua chanzo cha kupotea,mahali aliko na mtu ambaye wako naye,na pindi tu watasuluhisha, atajiunga na kikosi ambacho kimesafiri Ethiopia " Oguso alisema .

Aidha Oguso alisema kuwa kutokana na udukuzi wao, Hato yupo na mtu anayemjua. Hato alitarajiwa kukiongoza  kikosi cha timu hiyo ya Bullets ,katika michuano ya kujikatia tiketi kucheza kwenye CAF champions league , Ethiopia.

Aidha kutoweka kwake ni jambo ambalo liliwapa familia na marafiki  wake kipindi kigumu huku wakitoa ombi kupiga ripoti kwa atakaye muona.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved