Kocha wa klabu ya West Harm united inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza Julen Lopetegui sasa amemteua Jarrod Bowen kama nahodha mpya wa timu hiyo msimu huu mpya.
Bowen atakuwa akiridhi mikoba ya unahodha kutoka kwa aliyekuwa beki wa Chelsea Kourt Zouma baada ya kuhamia klabu ya Shabab ya uarabuni.
Bowen amekua mwiba katika safu ya uvamizi na kusaidia timu hiyo kutwaa taji la UEFA conference league mwaka wa 2023. Mzawa huyo wa Uingereza anatarajiwa kutamba sana wakati ligi kuu nchni humo inatarajiwa kuanza .Aidha, Bowen alifanya vyema katika kipute hicho na kuwa mchezaji bora katika mechi ya fainali ,vilevile ,mchezaji bora wa kipute hicho makala yaliyopita.
Bowen anadhihirisha uwezo wake baada ya kujumuishwa kwenye kikosi cha Uingereza kilichocheza kwenye makala ya yaliyopita ya Euro Ujerumani huku Taifa hilo likifika katika fainali na kulemewa na vijana wa Uhispania.
West Harm United ilifanikiwa kumaliza nafasi ya 14 msimu jana licha kusuasua na kupokea vipigo vya magoli mengi katika msimu huo,klabu hiyo sasa imejipanga vyema kwa msimu huja baada ya kufanya usajili wa majina tajika akiwemo mshambuliaji Fullkrug na beki Wan Bissaka kutoka Man United.