logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kinda wa Aston Villa Lamare Bogarde atia saini mkataba mpya

Unai Emery azidi kuimarisha kikosi chake,baada ya kupata ushindi mechi ya ufunguzi.

image
na Davis Ojiambo

Michezo19 August 2024 - 07:49

Muhtasari


  • •Lamare Bogarde  20 ametia wino mpya katika Aston Villa kipindi kisichojulikana ili kuisaidia timu hiyo katika ukabaji na kutafuta mabao.
LAMARE BOGARDE

Mholanzi na kinda anayechezea timu ya Aston Villa ,Lamare Bogarde ,20, ametia saini mpya katika klabu ya hiyo inayoshiriki katika ligi kuu nchni Uingereza .

Lamare alisajiliwa kutoka akademia ya klabu ya Feyeenoord timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18 ,na kusaidia timu hiyo ya Villa kunyakua ushindi katika  kombe la FA Youth cup dhidi ya liverpool U18  mwaka wa 2021.

Aidha ,kinda huyo ana tajiriba baada ya kuichezea timu ya Bristol Rovers inayoshiriki ligi ya daraja la kwanza. Vilevile ,Lamare ameweza kujumuishwa katika kikosi cha uholanzi  miaka minne na kuboresha taaluma yake ya kusakata mpira.

Mchezaji huyo ambaye timu ya Nottingham Forest ilikua imeonyesha jitihada za kumsajili na ambapo yeye mwenyewe alikataa na kuamua kusalia Villa Park kwa msimu mwingine ili kuboresha zaidi taaluma yake na vijana hao wa Unai Emery.

Aston Villa msimu uliopita walimaliza katika nafasi ya nne na kusajili nafasi ya juu zaidi tangia mwaka wa 1996 na kujikatia tiketi ya kucheza katika UEFA Champions League 2024/2025,chini ya ukufunzi wake Unai Emery.

Aston Villa katika mchakato wa kuwania taji msimu huu walipata ushindi baada ya kuibamiza timu ya West Ham United mabao 2-1 huku kiungo mpya kutoka timu ya Everton Amadou Onana akipachika bao lake la kwanza akichezea timu hiyo, huku mashabiki wa Villa wakimpongeza kwa matokeo bora katika mchuano huo na kunyakua pointi zote tatu nyumbani.Sasa Villa watawashika ugeni vijana wa Arsenali katika mchuano ufuatao tarehe 24  mwezi huu Villa Park.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved