logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Arsenali yamsajili Mikel Merino kutoka Real Sociedad

Arsenali yazidi kuimarisha kikosi kwa msimuu huku wakitarajiwa kucheza na timu ya Aston Villa wikendi hii.

image
na Davis Ojiambo

Michezo23 August 2024 - 10:27

Muhtasari


  • • Arsenali imekubali kumsajili kiungo raia wa Uhispania Mikel  Merino kutoka Real Sociedad kwa kima cha €37m.
  • • Ametia mkataba hadi mwaka 2028 na chaguo la kuongeza msimu ili kuisaidia timu hiyo ya Mikel Arteta ili kushinda taji kuu Uingereza na vile vile Champions League.
MIKEL MERINO

Klabu ya Arsenali inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza imemsajili kiungo Mikel Merino kutoka klabu ya Real Sociedad kwa kima cha €37m  kwa mkataba  wa hadi 2028 .

Merino ambaye ni mzawa wa Uhispania alisaidia Taifa hilo kunyakua ubingwa wa kombe la Euro mwaka huu mechi ambazo ziliandaliwa ujerumani.Ujio wake merino pale Arsenali utakuwa wa muhimu zaidi baada ya klabu hiyo kushindwa kubeba taji la ligi kuu nchini uingereza.  

Merino, ambaye ameichezea timu ya Sociedad kwa kipindi kirefu na kuisaidia kushinda kombe la  Copa del Rey mwaka wa 2020.Merino ambaye ashawashi kuwa nahodha katika klabu hiyo alianza taaluma yake katika klabu ya Osasuna.

Merino,ambaye ni mwanawe Angel Miguel ambaye alikuwa mchezaji wa timu ya Osasuna na pia vile vile mkufunzi katika klabu hiyo.

Vijana hao wa MikeL Arteta,sasa wamo mbioni kujikaza aghalabu kunyakua taji hilo baada ya kuwania taji hilo kwa zaidi ya misimu 19 bila kufanikiwa baada ya msimu huo wa 2003-04 ambapo walisha ligi bila kupoteza mechi hata moja.

Arsenali ,wanatarajiwa kutamba msimu huu baada ya kushinda mechi ya ufunguzi waliposhinda  mabao 2-0 dhidi ya Wolverhampton .Wikendi hii Arsenali watakuwa wanashuka dimbani kucheza na timu ya Aston Villa iliyosambaratisha hesabu zao ya kushinda ligi msimu jana baada ya kupigwa nyumbani na ugenini.

Aidha, Timu hiyo itakuwa inajiandaa kucheza katika kombe la Champions League.Merino atakuwa anasaidia timu hiyo katika safu ya katikati ili kuzalisha mabao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved