logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Endrick aweka rekodi kama mchezaji wa kigeni mdogo zaidi kufungia Real Madrid

Endrick sasa ameweka rekodi kuwa mchezaji mchanga zaidi kuwahi kuifungia timu hiyo na asiwe na usuli wa taifa hilo.

image
na Davis Ojiambo

Michezo26 August 2024 - 06:11

Muhtasari


  • • Endrick sasa ameweka rekodi kuwa mchezaji mchanga zaidi kuwahi kuifungia timu hiyo na asiwe na usuli wa taifa hilo.
  • •Endrick alisajiliwa na klabu ya Real Madrid kutoka Palmeiras na mechi ya Jumapili imekuwa mechi yake rasmi katika ligi hiyo .

Kinda Endrick Felipe Moreira de Sousa ambaye ni mzaliwa wa Brazil ,mwenye umriwa miaka 18 ambaye anachezea timu ya Real Madrid kwenye ligi kuu ya Uhispania, La Liga sasa ndiye mchezaji mdogo zaidi kutoka nche ya Uhispania kuwahi kuifungia timu hiyo.

Endrick, na ambaye pia huchezea timu ya taifa ya Brazil, alifunga bao siku ya Jumapili wakati timu ya Real Madrid ilikuwa inacheza na timu ya Valladolid alipoingia kama nguvu mpya kunako dakika ya 86 na kupata bao.

Mshambulizi huyo, alianza soka lake na kujulikana na wengi akiichezea timu ya Palmeiras akiwa na umri wa miaka 11 na kuchangia magoli mengi klabuni humo hadi alipoondoka.

Aidha, Endrick ndiye mchezaji mdogo zaidi kuwahi kujumuishwa katika kikosi cha taifa baada Ronaldo mwaka jana katika mashindano ya kutafuta tiketi ya kucheza katika kombe la Dunia mwaka jana.

Endrick alisajiliwa na klabu ya Real Madrid kutoka Palmeiras na mechi ya Jumapili imekuwa mechi yake rasmi katika ligi hiyo .

Endrick anarajiwa kutamba katika klabu ya mashabiki wa klabu hiyo kutokana na mchezo wake wa haiba licha ya umri wake mdogo.Endrick ambaye ameiga nyayo zake mchezaji wa timu hiyo wa zamani Christiano Ronaldo kutoka Ureno.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved