logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Orodha ya wachezaji wa soka ambao wamefunga mabao mengi kwa timu za taifa

Messi afikisha mabao 112 akichezea timu ya Argentina baada ya kufunga mabao matatu dhidi ya Bolivia

image
na jacob kimanthi

Michezo17 October 2024 - 13:02

Muhtasari


  • Christiano Ronaldo anaendelea kuongoza katika orodha ya wachezaji wenye mabao mengi wakichzea timu za taifa akiwa na mabao133 akichezea timu ya Ureno.

Christiano Ronaldo azidi kutamalaki katika safu ya ufungaji mabao akiwa na timu ya Ureno huku akiwa amepachika mabao 133.Mpinzani wake wa jadi Lionel Messi ajikakamua na kufikisha jumla ya mabao 112 baada ya kupachika mabao matatu wakati Argentina ikicheza na Bolivia.

Messi ambaye alipata jeraha  kiwiko cha mguu katika fainali ya CONMEBOL timu yake ikichukua ushindi dhidi ya Colombia kwenye mda wa ziada wa mechi,alirejea kwa kishindo huku akifunga mabo matatu na kutoa pasi iliyozalisha bao katika nafasi ya kuwania tikiti ya kucheza katika kipute cha CONMEBOL.

Mechi hiyo ilitamatika mabao sita kwqa sifuri huku wakiwa mabingwa watetezi katika taji hilo.

Mchezaji wa Napoli na taifa la Ubeligiji Romelu Lukaku,anatia fora katika oradha hii licha ya timu yake ya taifa kuwa na msururu wa matokeo duni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved