Gwiji wa Barcrelona na Argentina, Lionel Messi amefichua kwamba hana mpango wowote wa kuwa kocha pindi atakapostaafu kutoka soka.
Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 37 amekuwa akihusishwa na kufuata nyendo za malejendari wenza katika klabu ya Barcelona, akiwemo Pep Guardiola, Xavi Hernandez na hata Luis Enrique kuingia katika ukufunzi.
Hivi majuzi, Andres Iniesta alithibitisha nia yake ya kufuata nyayo zao, ingawa mtu mmoja ambaye hataki kufanya hivyo ni Lionel Messi.
Messi alizungumza na Fabrizio Romano wiki hii juu ya mada mbalimbali, na moja ilikuwa kuhusu mipango yake ya maisha baada ya soka kama mchezaji.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alithibitisha kuwa hana mpango wa kuingia katika usimamizi mara tu atakapostaafu. "Sina mpango wa kuwa meneja wakati nitastaafu.
Hili sio jambo ambalo ninafikiria kufanya." Inabakia kuonekana kama Messi ataendelea kujihusisha na soka wakati wote atakapotundika daruga zake.
Anaweza kurejea Barcelona kwa kiwango fulani, ingawa haionekani kuwa atafanya hivyo akiwa kocha mkuu wa kikosi cha kwanza. Kombe la Dunia la 2026 sio lengo rasmi la Messi, lakini mchezaji atalenga ikiwa ataendelea kucheza kwa furaha.
Messi amewahi kukiri kwamba nyota wa zamani wa Ufaransa Zinedine Zidane pia aliapa hatakuwa meneja, lakini hatimaye kuiongoza Real Madrid kushinda mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa.
Badala yake, Muargentina huyo amekiri kuwa angependa kuwa mkurugenzi wa michezo, akipendelea bila kushangazwa nafasi ya nyuma ya pazia ambayo ingempa usiri ambao amekuwa akitafuta katika maisha yake yote ya uchezaji akiwa na Barcelona, Paris Saint-Germain na Inter Miami.
Ripoti zinaonyesha kuwa mkataba wa Messi na Miami unajumuisha makubaliano kuhusu kuhusika kwake na klabu baada ya kustaafu kwake, ingawa maelezo ya kifungu hiki hayajawahi kuwekwa wazi.