Kocha wa timu ya taifa ya raga wa wachezaji saba maarufu kama Shujaa, ametaja kikosi cha wachezaji 13 wataoshiriki kwenye mashindano ya raga ya dunia HSBC 2024/2025 msururu wa Dubai.
Kocha wa timu hiyo Kelvin Wambua ametaja kikosi hicho kitachakoongozwa na George Ooro na Samuel Asati kama manahodha na ambacho kitasafiri kuelekea Dubai wiki lijalo Jumatatu, Novemba 25.
Kwenye kikosi cha kocha Wambua, Brayan Ondego amejumuishwa kwa mara ya kwanza kikosini humo kushiriki mchezo wa kwanza wa HSBC 2024/2025.
Wachezaji wengine ambao wamejumuishwa kikosini humo ni Kevin Wekesa, William Mwanji, Brian Mutua, Dennis Abukuse, Nygel Amaitsa, Chrisant Ojwang, Patrick Odongo, Festus Shiasi, Benson Salem na Floyd Wabwire.
Kikosi hicho baada ya kumaliza msururu wa Dubai, kitaelekea nchini Afrika Kusini kwa mechi za mkondo wa pili.
Jumla ya timu 24 zitashiriki msururu wa Dubai Sevens katika uwanja wa Sevens Stadium kuanzia Novemba hadi Desemba Mosi kisha kusafiri nchini Afrika Kusini kushiriki mkondo wa pili kuanzia Desemba 7 hadi Desemba 8.
Baada
ya kukamilika kwa misururu ya Dubai na Cape Town mwaka huu, ligihiyo ya HSBC
itaendelea mwaka ujao misururu ikiratibiwa kuendelea Perth, Vancouver na
hatimaye Hong Kong.