logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nahodha wa Chelsea, Reece James apata jeraha lingine tena!

Kabla ya pambano la Jumamosi, Maresca alithibitisha wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya mechi siku ya Alhamisi kwamba James amepata jeraha la misuli ya paja.

image
na MOSES SAGWEjournalist

Michezo21 November 2024 - 15:34

Muhtasari


  • Ni pigo kubwa kwa James, ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji waliopigwa picha akifanya mazoezi na wachezaji wengine wa kikosi cha Chelsea mapema wiki hii.
  • Nahodha huyo wa The Blues amecheza mara nne pekee katika kampeni hii, akicheza kwa dakika 241 kwenye Premier League.



Mkufunzi wa Chelsea Enzo Maresca amefichua kuwa Reece James atakosa mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Leicester City wikendi.

The Blues watamenyana na Foxes katika mechi ya kwanza ya Jumamosi mchana, huku Maresca akirejea King Power Stadium kwa kikosi cha kwanza tangu alipoondoka na kujiunga na Chelsea kama mrithi wa Mauricio Pochettino.

Umekuwa mwanzo mzuri kwa Muitaliano huyo hadi sasa Magharibi mwa London, huku Chelsea kwa sasa wakiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Kabla ya pambano la Jumamosi, Maresca alithibitisha wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya mechi siku ya Alhamisi kwamba James amepata jeraha la misuli ya paja.

Maresca alisema: "Tuna mchezaji mmoja tu aliyeumia, huyo ni Reece. Kwa bahati mbaya alihisi kitu kidogo na hatutaki kuchukua hatari yoyote kwa wikendi."

Muitaliano huyo aliongeza: "Hamstring. Ni tatizo la misuli. Hatutaki kujihatarisha kwa wikendi hii. Tunatumai si jambo refu."

Ni pigo kubwa kwa James, ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji waliopigwa picha akifanya mazoezi na wachezaji wengine wa kikosi cha Chelsea mapema wiki hii.

Nahodha huyo wa The Blues amecheza mara nne pekee katika kampeni hii, akicheza kwa dakika 241 kwenye Premier League.

Maresca alithibitisha kwamba James alipata jeraha hilo siku ya Jumanne, huku kocha wa Chelsea kwa sasa akiwa hana uhakika ni muda gani mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 atakaa nje ya uwanja.

"Alihisi kitu, lazima awe nje. Kwa hakika, wikendi hii na kisha tutaona. Hatujui kwa muda gani," Maresca alisema.

"Lazima ajaribu kuepuka kadri awezavyo lakini wakati mwingine mambo hutokea hata kama unataka kuepukana na hilo. Tunatumai anaweza kupatikana kwa anayefuata lakini hapatikani kwa hili."

James tayari amekosa sehemu kubwa ya msimu huu kutokana na jeraha la misuli ya paja na bado haijafahamika iwapo atarejea kwenye kikosi cha The Blues kwa ajili ya mechi yao ijayo ya Ligi Kuu dhidi ya Aston Villa Jumapili, Desemba 1.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved