logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanariadha atakayevunja rekodi ya Kelvin KIptum kwenye Valencia Marathon kutuzwa Ksh 135m

Wanariadha 3 kutoka Kenya wanatarajiwa kushiriki katika kitengo cha wanaume katika mbio za marathon; Sabastian Sawe, Hillary Kipkoech na Daniel Mateiko.

image
na MOSES SAGWEjournalist

Michezo27 November 2024 - 10:41

Muhtasari


  • Rekodi za sasa za ulimwengu katika kategoria za wanaume na wanawake zinashikiliwa na Wakenya.
  • Ruth Chepngetich anashikilia rekodi ya wanawake baada ya kuweka rekodi ya mwendo wa 2:09:56 katika mbio za 2024 za Chicago Marathon.
  • Rekodi ya wanaume inashikiliwa na marehemu Kelvin Kiptum.



Waandalizi wa mbio za marathon za mjini Valencia wametoa dau nono la hadi shilingi milioni 135 pesa za Kenya kwa mwanariadha yeyote atayakevunja rekodi vya dunia inayoshikiliwa na hayati Kelvin Kiptum.

Mbio hizo zitafanyika Desemba 1 katika jiji la Valencia nchini Uhispania kuanzia majira ya saa nne asubuhi.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, waandalizi wametangaza zawadi ya taslimu ya shilingi milioni 135 kwa mwanariadha yeyote atakayevunja rekodi ya Kiptum ya 2:00:35.

"Tunataka kutangaza kwamba atakayevunja rekodi ya dunia atapata euro milioni moja, ikiwa atavunja huko Valencia, bila shaka. Paco Borao atatoa nusu moja nami nitampa nusu nyingine," alisema Juan Roig, mwandalizi mwenza wa mbio hizo.



Wanariadha 3 kutoka Kenya wanatarajiwa kushiriki katika kitengo cha wanaume katika mbio za marathon; Sabastian Sawe, Hillary Kipkoech na Daniel Mateiko.

Sadfa ni kwamba Wote watatu wamepangwa kuanza marathon yao ya kwanza.

Rekodi za sasa za ulimwengu katika kategoria za wanaume na wanawake zinashikiliwa na Wakenya.

Ruth Chepngetich anashikilia rekodi ya wanawake baada ya kuweka rekodi ya mwendo wa 2:09:56 katika mbio za 2024 za Chicago Marathon.

Rekodi ya wanaume inashikiliwa na marehemu Kelvin Kiptum.



Utendaji wa Kiptum katika mbio za Chicago Marathon za 2023 zilipamba vichwa vya habari duniani. Muda wake wa mbio za chini ya 2:01 wa marathon sio tu kwamba aliweka rekodi mpya ya ulimwengu lakini pia alimweka kijana mwenye umri wa miaka 24 kama mmoja wa vipaji vya kuahidi katika historia ya marathon.

Hata hivyo, alikufa kwa kusikitisha katika ajali ya gari mnamo Februari na hivi karibuni aliadhimishwa na ukumbusho wa kuhakikisha urithi wake unaishi katika mitaa ya Chicago.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved