KILA kitu kinaonekana
kwenda kombo kwa Roma msimu huu - klabu hiyo ya Serie A hata imeandika vibaya
jina la mchezaji wao kwenye jezi yake.
Katika kipigo cha mabao
2-0 kutoka kwa Atalanta siku ya Jumatatu, mshambuliaji wa Ukraine Artem Dovbyk
alikuwa na jina la ‘Dobvik’ mgongoni.
Mitandao ya kijamii
ilisambaratika na gazeti la michezo la Roma Corriere dello Sport lilisema
Jumanne kwamba kosa hilo "halikuwa la kuaminika," huku Tuttosport
ilisema ni "kosa la dalili kwa Warumi hao waliochanganyikiwa."
Klabu hiyo ya Roma
tayari imekuwa na makocha watatu msimu huu na inashika nafasi ya 15. Beki wa
Ujerumani Mats Hummels amevumilia mwanzo mgumu katika kipindi chake cha kucheza
Giallorossi na kuchechemea dhidi ya Atalanta.
Wakiwa na makocha watatu
katika mechi 14 za Serie A na wameshinda pointi 13 pekee, Roma wana msimu wa
kusahau. Na katika kushindwa kwa Atalanta Jumatatu hii, makosa ya uwanjani pia
yaliongezeka hadi... vifaa.
Fowadi huyo wa Ukraine
amefunga mabao sita katika mechi 18 alizoichezea Waroma msimu huu.
Wakishika nafasi ya 15
kwenye Serie A, Roma wana pambano na Lecce siku ya mechi ijayo, kati ya timu
mbili ambazo bila kutarajia zina alama 13 sawa.
Fowadi huyo mwenye umri
wa miaka 26, ambaye alijiunga na Roma kutoka Girona msimu huu wa joto kwa Euro
milioni 30.5, bado hajatimiza matarajio.
Kufikia sasa, Dovbyk
amefunga mabao sita na kutoa asisti moja katika mechi 18 katika mashindano
yote. Ingawa mchango wake unaheshimika, wanapungukiwa na matumaini makubwa
waliyonayo Roma kwa usajili wao wa majira ya kiangazi.
Kabla ya kujiunga na
Girona mnamo 2023, Dovbyk alichezea vilabu vikiwemo Dnipro, Zorya, Midtjylland,
na SønderjyskE. Hata hivyo, msimu wake wa kwanza nchini Italia umegubikwa na
misukosuko ya timu na hitilafu hii ya hivi punde nje ya uwanja.