Kocha wa Manchester United Ruben Amorim amedai kuwa
timu yake ni "klabu kubwa lakini si timu kubwa" na amesisitiza
kiwango chao cha kufanya kazi nje ya mpira kama eneo ambalo linahitaji
kuboreshwa.
United walipata ushindi mara mbili katika mechi tatu
za ufunguzi za Amorim akiwa kocha wa klabu - dhidi ya Bodo/Glimt na Everton -
lakini wakapata kipigo chao cha kwanza chini ya bosi mpya dhidi ya Arsenal
katikati ya wiki.
Mabao kutoka kwa Jurrien Timber na William Saliba
yaliipatia timu ya Mikel Arteta ushindi wa 2-0, huku United sasa ikishuka hadi
nusu ya mwisho ya jedwali la Ligi Kuu kabla ya mechi yao ijayo dhidi ya
Nottingham Forest, Jumamosi.
Kabla ya mchezo huo, Amorim alizungumza kwa uwazi
kuhusu matatizo yanayoikumba timu yake na kazi kubwa ya kufanya kabla ya United
kuwa miongoni mwa vigogo wa soka duniani kwa mara nyingine tena.
Alisema: "Hilo liko wazi. Sisi ni klabu kubwa,
lakini sisi si timu kubwa. Tunaijua, hivyo si tatizo kuisema. Tunapaswa kuamini
zaidi.”
"Tuna
mambo mazuri, lakini unaweza kuhisi kwamba kuna mengi ya kufanya. Tunapaswa
kuwa bora zaidi katika tatu ya mwisho."
Alipoulizwa ikiwa mashabiki watahitaji kupunguza
matarajio yao katika siku za usoni, Amorim aliendelea: "Hilo halitabadilika
kutokana na utukufu wa hapo awali.”
"Wachezaji
wetu wanapaswa kuelewa kwamba ni nafasi ngumu. Sisi sio timu bora kwenye ligi,
lakini zamani zetu ni bora zaidi kwenye ligi.”
"Tuna tatizo, lakini tunapaswa kuzingatia
maelezo madogo."
Jambo dogo ambalo amedhamiria kulifanyia kazi ni
utimamu wa wachezaji wake.
United inashika nafasi ya sita ya mwisho ya Ligi ya
Premia kwa umbali wa wastani unaotumika na Amorim sasa amefanya jukumu lake
kuboresha kiwango chao cha kufanya kazi nje ya mpira kupitia uwanja wa mazoezi.