logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Eliud Kipchoge aahidi kurejea kwa kishindo katika riadha zitakazoandaliwa mwaka ujao

Kipchoge sasa ameanza safari ya kujiboresha na kufanya matayarisho kwa ajili ya mashindano ya mwaka ujao

image
na OTIENO TONNY

Michezo11 December 2024 - 15:21

Muhtasari


  • Kipchoge  ameanza safari ya kujiboresha na kufanya matayarisho kwa ajili ya mashindano ya mwaka ujao.
  • Licha ya kushindwa katika mbio za olimpiki Paris Kipchoge bado anajivunia kuwa mshindi wa mara tano wa Berlin Marathon na mshindi wa Olimpiki mara mbili mtawalia. 


Mwanariadha wa masafa marefu tajika ulimwenguni Eliud Kipchoge ameonyesha kukubaliana na changamoto alizokumbanana nazo katika Olimpiki ya Paris nchini Ufaransa ya mwaka 2024.

Kipchoge sasa ameanza safari ya kujiboresha na kufanya matayarisho kwa ajili ya mashindano ya mwaka ujao. Nyota huyo wa riadha  sasa anapania kuwashawishi na kuhamasisha wengine akipania kurejea katika mashindano baada ya kuchukua likizo fupi.

Licha ya kushindwa katika mbio za Olimpiki Paris, Kipchoge bado anajivunia kuwa mshindi  mara tano wa Berlin Marathon na mshindi wa Olimpiki mara mbili mtawalia. Juhudi zake za kutwaa ubingwa kwa mara ya tatu katika olimpiki iligonga mwamba. Hata hivyo mwanariadha huyo amesema kuwa hata kata tamaa katika azimio lake kwani anapania kurejea katika mashindano kwa nguvu mpya mwaka ujao wa 2025.

Mwanariadha huyo aliashiria kuwa upendo alionao katika masuala ya michezo ndio chanzo kikuu kinachompa motisha ya kurudi tena katika mashindano na kuwapatia vijana chipukizi motisha na kuwashawishi kutokata tamaa hata wanapokumbwa na changamoto.

‘’Michezo ni kuhusu kujituma, kusukuma na kusukuma kila siku na hiyo ndiyo maisha, kuna vitu ambazo hufanyika katika maisha yetu ambazo hatuwezi kuepuka. Nilichukua likizo fupi baada ya mashindano ya olimpiki pari na baadaye nikarejea kufanya zoezi ndio maana  maisha yamekuwa mazuri na ya kuridhisha,’’ Alisema Kipchoge akihojiwa na shirika la habari la China Daily.



Kipchoge ambaye ameandika historia kama mwanariadha bora duniani katika mbio za masafa marefu alisema kwamba bado ana matumaini ya kuendelea kushiriki katika mashindano akisisitiza kuwa kufanya jambo mara mingi ndio siri ya kuwa bora katika kila jambo.

‘’Siri ni kufanya jambo na kurudia hilo jambo mara mingi zaidi ndiposa ubora uonekane, mimi nimekuwa nikifanya mazoezi kila siku naamka asubuhi na kukimbia na kadri nilipokuwa nikifanya mazoezi ndio misuli zangu zilipata mazoea ya mazoezi. Kile ninachokijivunia zaidi ni kuvunja rekodi ya kukimbia chini ya masaa mawili na kuwafahamisha wanariadha wengine kuwa binadamu hana kikomo wala upungufu,’’ Alisema  Kipchoge.

Mwanariadha huyo alisema kuwa utamu wa kushiriki katika riadha si kuvunja rekodi na kuibuka mshindi pekee bali pia ni kupata furaha na kujiridhisha moyoni wakati unapomaliza mbio akiongeza kuwa lengo kuu la riadha ni kumaliza hata kama ni kwa kutembea wala si kushindana pekee.

Kipchoge amewataka  mashabiki wake na mashabiki wa riadha ulimwenguni wawe tayari kumwona na kumshangilia tena mwaka ujao akishiriki katika mashindano mbalimbali za riadha. Hii ni baada ya kuwahakikishia wafuasi wake kuwa baada ya kuchukua likizo fupi sasa amerejea kufanya maandalizi kwa ajili ya mwaka ujao.


 



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved